Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kilindi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyamamu(mwenye 'track suit') akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Majjid Mwanga. |
Mwenge wa uhuru mwaka 2014
umeweka jiwe la msingi katika chumba cha upasuaji mdogo kilichojengwa katika
zahanati ya Majengo iliyopo kata ya Manundu mjini Korogwe.
Akisoma taarifa ya mradi kabla ya
kuwekewa jiwe la msingi na Mkimbiza
Mwenge kitaifa Rachel Kassanda, Mganga Mkuu wa halmashauri ya mji Korogwe Dkt
Jerry Mwakanyamale alisema kuwa mradi huo ulioanza kujengwa mwaka 2013 kwa
fedha za bajeti ya CDG na MMAM mpaka sasa umegharimu jumla ya Tsh.21,048,410/-
Aliongeza kuwa mwaka wa fedha
2012/2013 mradi huo ulitengewa jumla ya Tsh.34,147,000 zikiwa ni CDG Tsh.24,100,000/-
ambapo Tsh .18,000,000/- zimeshaletwa na Serikali wakati MMAM ilitengwa Tsh
10,047,000 na fedha zote zimeshatolewa.
Dkt Mwakanyamale alifafanua mpaka
sasa ujenzi huo ili kukamilika umebakisha vyumba 2 vya kubadilishia nguo
kabla ya kuingia chumba cha upasuaji,vyoo viwili na korido la kusubiria
wagonjwa wakiwa 'theatre'
Wakizungumza na Mwandishiwa
habari katika mahojiano maalumu baadhi
ya Wananchi waliohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi katika zahanati hiyo,
walisema kuwa wanaishukuru sana Serikali kwa kuzidi kuwasogezea huduma za afya
jirani na makazi yao na kuongeza kuwa wana imani chumba hicho cha upasuaji mdogo kitakuwa
msaada mkubwa kwao katika masuala ya afya.
"Hii 'theatre' itatusaidia
sana hasa ukizingatia kuwa Korogwe imekuwa ikikumbwa na ajali nyingi za
barabarani kwa kuwa ni njia kuu ya miji mikuu ya Tanzania,hivyo itaipunguzia
mzigo Magunga".Alisema Asha Hassan mkazi wa Manundu.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
wilaya ya Korogwe Dkt Rashid Said alisema kuwa chumba hicho cha upasuaji mdogo
kitaisaidia sana wilaya yake kwani kitapunguza msongamano katika hospitali ya Magunga kwa kuwa wagonjwa wengi wa upasuaji mdogo,kufungwa na kusafishwa vidonda,walioumia
katika ajali wataweza kupata huduma katika 'thearter' hiyo ya zahanati ya Majengo pindi itakapokamilika tofauti na
sasa ambapo Magunga huhudumia wagonjwa wote na hivyo kuwa na mzigo mkubwa sana
hasa zinapotokea ajali za barabarani.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Majjid Mwanga akimkaribisha kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Rachel Kassanda wilayani Korogwe (Kilole),akitokea wilaya ya Kilindi. |
EmoticonEmoticon