Mwenyekiti
wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi
(katikati-meza kuu) akiwa na wajumbe wa Kamati hiyo wakati walipokuwa
wanawahoji waomba hifadhi (hawapo pichani) katika Kambi ya Wakimbizi ya
Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao
wanatoka nchi mbalimbali ambapo wengi wao ni Wakongo. Zaidi ya waomba
hifadhi 300 wanahojiwa na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane
za Serikali ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP),
Idara ya Wakimbizi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri
Kiongozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya
Inspekta Jererali wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la
Kimataifa ya Kuhudumia Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti
wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi
(watatu kushoto), Katibu wa Kamati hiyo, Philo Nombo (watatu kulia)
ambaye anamwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, wakiwa
katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo baada ya kuwahoji
waomba hifadhi katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya
Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi mbalimbali ambapo
wengi wao wanatoka nchini Kongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanaendelea
kuhojiwa na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali
ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya
Wakimbizi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri
Kiongozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya
Inspekta Jererali wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la
Kimataifa ya Kuhudumia Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
EmoticonEmoticon