Magari yakivuka juu ya daraja la
muda la Mto Kilombero lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja
la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe
za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.
PICHA NA IKULU
Magari yakivuka juu ya daraja la
muda la Mto Kilombero lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja
la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe
za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akipungia wananchi kwa furaha wakati akielekea ukingoni mwa Mto
Kilombero kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto
Kilombero Agosti 20, 2014. Anaoongozana nao ni pamoja na Waziri wa
Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe.
Celina Kombani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera
(kushoto) na Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la
kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Pamoja naye ni Waziri wa
Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe.
Celina Kombani (kulia), Mbunge wa Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais),
Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero
Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akipata maelezo toka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Bw.
Patrick Mfugale juu ya ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero
Agosti 20, 2014. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe, Magufuri
akifuatiwa na Mama Salma Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada ya kuweka
jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero
wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja
la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro
Agosti 20, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akijaribu madawati mapya ya shule ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge
baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya
Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya
Graphite na Nickel mkoani wa Morogoro Agosti 20, 201
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
mkewe Mama Salma Kikwete na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi ya
Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa
madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na
uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani Morogoro Agosti
20, 2014.
EmoticonEmoticon