Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Arusha
Robinson Meitinyiku akitoa taarifa ya ufafanuzi kwa waandishi wa habari
juu ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari
na baadhi ya viongozi wa UVCCM mkoani hapa. Ambao Mkutano huo
ulitanguliwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha waliaofikiana
kutoa maamuzi juu ya mgogoro wao na Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha
Gerald Mwadalu anayetuhumiwa kufunga ofisi na matumizi mabaya ya fedha
za umoja huo.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Karatu
Ally Rajabu akisoma maazimio ya Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa
Arusha lililokutana leo na kutoa maazimio 17 likiwamo la kumpiga
marufuku Kaimu Katibu UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu asijihusishe
na kazi za UVCCM mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa UCVVM Mkoa wa
Arusha Robnson Meitinyiku na baadhi ya wajumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa
wa Arusha wakisikiliza maazimio yaliyopitishwa na wajumbe wakati
yalipokuwa yakisomwa mbele ya waandishi wa habari mjini hapa
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji
wa UVCCM Mkoa wa Arusha Diwani Kimayi katikatika pamoja na wajumbe
wenzake wakisikiliza maazimio yaliyokuwa yakisomwa ambapo kwa upande
wake alitoa ushauri kwa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kwamba linapoteua
watendaji lie linaangalia watendaji wenye sifa.
Sehemu ya mkutano wa waandishi
wa habari na wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM mkoa wa Arusha
kikiendelea leo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Rose
EmoticonEmoticon