Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
13/08/2014
Serikali
imetenga fedha zitagawiwa kwenye vituo vyote vinavyotoa ushauri nasaha
na kurekebisha watoto walio chini ya umri wa miaka 18 vilivyo chini ya
Idara ya Ustawi wa jamii nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Nsachris Mwamwaja kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti la Majira
toleo Na. 7524 Vol.II/5624 la Jumatano Agosti 13, mwaka huu yenye kichwa
cha habari “Mahabusu ya watoto yadaiwa mil. 1/=”.
“Ni
kweli tatizo hilo lipo ndio maana Serikali imetenga fedha tayari ambazo
zitagawiwa kwenye vituo vyote nchi nzima” alisema Mwamwaja.
Mwamwaja alisisitiza kuwa deni hilo litalipwa kweye mahabusi hiyo iliyoko Tanga.
Mahabusi
hiyo ni miongoni mwa vituo kadhaa vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa
Jamii ndani ya Wizara ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Matumizi
ya fedha hizo ni pamoja na kushughulikia tatizo la maji na uhaba wa
chakula kituoni hapo ili kuendelea kutoa huduma stahiki kwa watoto hao
na kufikia lengo la kuwarekebisha tabia zao ili wawe raia wema nchini.
Aidha,
Mwamwaja aliongeza kuwa fedha zilizotengwa si za Mkoa wa Tanga tu bali
ni kwa ajili ya vituo vya nchi nzima zikiwemo makambi ya wazee
wasiojiweza, mahabusi za watoto na kambi za kutibu wagonjwa wa ukoma.
EmoticonEmoticon