Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chuo cha Nelson Mandela cha
jijini Arusha wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua Kongamano la
Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za
Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. (Picha na
OMR).
Kongamano
hilo la siku tatu limefanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na
Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Jijini Arusha Agosti 5, 2014, na
kushirikisha mabingwa mbalimbali wa tafiti ndani ya Afrika na nchi za
ukanda wa Jangwa la Sahara.
Kongamano
hilo ambalo limedhaminiwa na Shirika la misaada la Kimataifa la
Marekani (USAID) linalenga kukuza tafiti za kisayansi na kutanua
maendeleo ya tafiti hizo ili yasaidie wananchi wa nchi za ukanda huu
hasa vijana ambao wanaelezwa kuwa na idadi kubwa kulinganisha na wazee
na akina mama.
Katika
Hotuba ya mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alisema kuwa, dhana ya umuhimu
katika uwekezaji na utanuaji wa sayansi katika Afrika, inahitaji
kutazama kundi la vijana na kulihamasisha kushiriki katika masomo ya
sayansi ili kuharakisha maendeleo kwa Bara la Afrika.
Makamu
wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika
Chuo cha Nelson Mandela, Bernard Mussa, aliyetafiti kuhusu kuongeza
joto katika Majiko kwa kutumia mwanga wa jua, wakati Dkt. Bilal
alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la
siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na
uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa
la sahara.
Makamu
wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi wa Masai Stove’s
& Solar, Kisioki Moitiko aliyetafiti kuhusu mzunguko wau meme wa Jua
kutumika katika nyumba za kabila la kimasai (Maboma) wakati Dkt. Bilal
alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la
siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na
uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa
la sahara.
Makamu
wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Hassna Founoune, kutoka Taasisi ya
Tafiti ya Kilimo ya Senegal, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo
kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la
kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za
Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu
wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa jambo katika Screen na Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson
Mandela, Prof. Bulton Mwamila, wakati wakiangalia mjadala uliokuwa
ukiendelea kupitia ‘Video Conference’ kati ya Marekani na Tanzania,
kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na
uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa
la sahara.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi.
EmoticonEmoticon