LHRC YATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YA NUSU MWAKA KUANZIA JANUARY HADI JUNI 2014

July 31, 2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba
Mtafiti wa Tafiti mbalimbali wa LHRC, Wakili Pasience Mlowe.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leoasubuhi, wakati akitoa taarifa ya kituo hicho ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari hadi kufikia Juni 2014. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio na Mtafiti wa LHRC, Pasience Mlowe.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwachua picha za utoaji wa taarifa hiyo.
Mtafiti wa Tafiti mbalimbali wa LHRC, Wakili Pasience Mlowe (kushoto), akisoma taarifa hiyo kwa wanahabari. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba
Wanahabari wakiwachua picha za utoaji wa taarifa hiyo. Imeandaliwa na www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 
Dotto Mwaibale
 
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kuwa hadi kufikia Juni 2014 wanawake na wasichana 2878 wamebakwa nchini kutokana na vitendo vya ukatili dhidi yao.
 
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba wakati akitoa taarifa ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari na Juni mwaka huu kwa vyombo vya habari Dar es Salaam leo.
 
“Vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya makundi hayo vilivyoripotiwa polisi kwa nchi nzima vilikuwa 3,633″ alisema Kijo -Bisimba.
 
Kijo-Bisimba alisema taarifa hii inatoka na tafiti zilizofanywa na kituo hicho ili kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka kwa waangalizi wa haki za binadamu, wasaidizi wa sheria, taarifa rasmi kutoka taasisi za Serikali, Bunge, Mahakama,vyombo vya habari na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali.
Akizungumzia kuhusu taarifa ya Sensa ya watu na makazi inaonesha idadi kubwa ya watu wanaishi vijijini huku wakiwa na huduma duni za kijamii kama za afya, maji, umeme, umeme na shule.
 
Alisema takwimu zinaonesha bado vijijini kuna makazi duni ya wananchi kutokana na gharama kubwa za saruji na vifaa vya ujenzi, mfano katika suala la upatikanaji maji makazi 3,959,857 yanatumia vyanzo vya maji visivyo salama ukilinganisha na makazi 1,902,244 yanayotumia maji ya bomba nchi nzima.
 
Kuhusu kilimo alisema idfadi ya wananchi wengi wapatao 11,359,090 wanategemea kilimo kama shughuli kuu ya uchumi hata hivyo wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono.
 
“Uwekezaji katika mashamba makubwa wamepewa wawekezaji wakubwa mfano mashamba makubwa ya mpunga yaliyokuwa ya Shirika la NAFCO wilayani Mbarali mkoani Mbeya wamepewa wawekezaji na wakulima wazawa wametengewa yasiyofaa” alisema Kijo-Bisimba.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »