WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
NDUGU
WANAHABARI, MTAKUMBUKA KUWA WIKI MOJA ILIYOPITA JESHI LA POLISI LILITOA
TAARIFA KWA UMMA JUU YA WATUHUMIWA SITA WALIOKAMATWA NA KUFIKISHWA
MAHAKAMANI KUHUSIANA NA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA TAREHE
07/07/2014 KATIKA MGAHAWA WA VAMA ULIOPO MAENEO YA VIWANJA VYA GYMKANA
JIJINI ARUSHA.
TAARIFA
HIYO ILIZUNGUMZIA PIA TUKIO LA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE
BAADA YA KUPEKULIWA NYUMBANI KWAKE ALIKUTWA NA MABOMU SABA YA KURUSHA
KWA MKONO, RISASI SITA ZA BUNDUKI AINA YA SHOT-GUN PAMOJA NA UNGA WA
BARUTI. TULIELEZA PIA KUWA OPERESHENI YA KUKAMATA WATUHUMIWA WENGINE
KUHUSIANA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI ILIKUWA
IKIENDELEA, NA KWAMBA WATUHUMIWA KADHAA WALIKUWA CHINI YA ULINZI WA
POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO HAYO.
KUTOKANA
NA OPERESHENI HIYO ENDELEVU, WATUHUMIWA WENGINE KADHAA WAMEKWISHA
KAMATWA NA KUHOJIWA, AMBAPO USHAHIDI ULIOKUSANYWA UMEBAINI KUWA KATI
YAO WATUHUMIWA ISHIRINI NA MOJA (21) WANAHUSIKA KATIKA MATUKIO
MBALIMBALI YA ULIPUAJI MABOMU NA KUMWAGIA WATU TINDIKALI HAPA JIJINI
ARUSHA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA MWAKA 2012 HADI YALE YALIYOTOKEA
KATIKA KIPINDI CHA HIVI KARIBUNI. WATUHUMIWA HAO WANATAZAMIWA KUFIKISHWA
MAHAKAMANI TAREHE 01/08/2014 KUUNGANA NA WENZAO WALIOKWISHA TANGULIA
ILI KUJIBU MASHITAKA YANAYOWAKABILI. UFAFANUZI WA WATUHUMIWA
WALIOKAMATWA NA MATUKIO WALIYOHUSIKA NAYO NI KAMA IFUATAVYO:
EmoticonEmoticon