WABUNGE VIJANA ,JOSHUA NASSARI NA STEPHEN MASELE KUKUTANA NA RAIS OBAMA LEO.

July 28, 2014


Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari  akizungumza wakati wa tafrija ya chakula cha jioni baada ya maafali ya kuhitimu mafunzo ya wiki tisa kwa viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika yaliyokuwa yakifanyika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani ,
Hotuba ya Mh,Nassari ilionekana kuwagusa wageni mbalimbali katika tafrija hiyo na wengine kushindwa kujizuia na kuanza kutokwa na machozi.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na Mstahiki Meya wa Fayetteville Arkansas ,Lioneld Jordan.
Wahitimu ,viongozi vijana toka nchi mbalimbali Afrika.
Ratiba ya Viongozi vijana toka nchi mbalimbali barani Afrika ambayo inaonesha leo hii wahitimu hao akiwemo Mh Joshua Nassari na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele wanakutana na Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama na baadaye jioni kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,John Kerry.Masele alikuwa chuo kikuu cha Florida na Nassari alikuwa chuo kikuu cha Arkansas.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »