Dkt.Jakaya Kikwete na Mkurugenzi
Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge
Corporation Bwana Karl Fickensher wakifunua kitambaa katika jiwe la
msingi Kuzindua Barabara ya Lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa
kilometa 71.4 iliyojengwa kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia mfuko
huo wakati wa hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani
Namtumbo leo.
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za
millennia(Millenium Challenge Corporation Bwana Karl Fickensher wakati
wa uzinduzi wa Barabara ya lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa
kilometa 71.4 iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania
na msaada kutoka kwa watu wa Marekani kupitia mfuko huo katika sherhe
zilizofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo Mkoani
Ruvuma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimwagilia maji mti wa kumbukumbu aliupanda muda mfupi baada ya
kuzindua barabara ya Songea hadi Namtumbo yenye urefu wa kilomita 71.4
katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo
leo. Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Watatu
ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile, Wanne ni
Mkurugenzi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania Bwana Bernard
Mchomvu,Wapili kulia ni mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa na kulia ni
Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Bwana Karl
Fickenscher.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete,Balozi Mdogo wa Japan Bwana Kazuyoshi Matsunaga(katikati) na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(African Development
Bank) ADB Bibi Tonia Kondiero kulia wakifunua kitambaa katika jiwe la
msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Lami ya Namtumbo- Matemanga
yenye urefu wa kilomita 128.9 uliofanyika katika kijiji cha Migelegele
.Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli na watatu
kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Barabara hiyo inajengwa na
serikali ya Tanzania ikisaidiwa na fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya
Afrika na serikali ya Japan kupitia shirika lake la misaada la JICA.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi
wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali mpya ya wilaya ya Namtumbo
Mkoani Ruvuma uliofanyika jana.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana
Saidi Mwambungu.(picha na Freddy Maro)
Rais Kikwete aliposimama katika
kijiji cha Utwango kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea mjini
Namtumbo akitokea Songea mjini
EmoticonEmoticon