Akizungumza kwa njia ya simu na TANGA RAHA BLOG,Meneja wa Akudo Impact,Juma Abajalo alisema maandalizi ya kuelekea bonanza hilo lililopewa jina la Shangwe za sikukuu ya Iddi limekamilika kwa asilimia kubwa.
Abajalo alisema wapenzi wa mziki wa dansi hapa nchini wakae mkao wa kula wakisubiria burudani kabambe itakayotolewa na wasanii wanaounda bendi hiyo maarufa hapa nchini wakiwemo Taasisi Masela Zegrebu Butam,Alen Kabasele mtoto wa pepekale Dipron aliyekuwa malaika bendi na Rap Fadii.
Alisema baada ya kumalizika onyesho hilo la Msasani Beach bendi hiyo itaondoka usiku kuelekea Visiwani Zanzibar Iddi Pili na siku Ijumaa inayofuata watahamia kufanya onyesho lao katika ukumbi wa Hiltech Banana Ukonga na Jumamosi watafanya kwenye ukumbi wa Cheetozi Miti Mirefu Sayansi.
Aidha alisema budurani zote hizo zitakuwa ni za kiwango cha hali ya juu na kuwataka wapenzi wa mziki huo kujitokeza kwa wingi kushuhudia maonyesho hayo yatakayokuwa gumzo mara baada ya kumalizika mfungo mtukufu wa ramadhani.
Hata hivyo alisema katika kuhakikisha onyesho hilo warembo
watakaokonga nyoyo wapenzi watakaojitokeza wataongozwa na Mrembo Raisa ambaye amekuwa akifanya vizuri sana hasa anapokuwa stejini.
EmoticonEmoticon