NA SAID KARSANDAS,
MOROGORO.
MABINGWA wa soka Tanzania bara 1988 African Sports
“Wanakimanumanu” leo wameanza vema michuano ya Ligi ya Mabingwa wa mikoa mara
baada ya kuibamiza Kiluvya United bao
1-0 mchezo uliochezwa kwenye dimba la soka Jamhuri mkoani hapa.
Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani wa hali
ya juu ambao mpaka timu zote zinakwenda mapumziko hakuna timu iliyoweza kuona
lango la mwenzake ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi.
Wakionekana kujipanga baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi
ya wachezaji wake,African Sports waliweza kucheza vema wakiwa na wachezaji wake
mahiri waliowasajili msimu huu.
Ilikuwa ni dakika ya 76 mashabiki wa timu ya African Sports
walipoinuka kwa shangwe na nderemo kutokana na shuti kali lililopigwa na James
Mendy na kuzama wavuni.
Akizungumzia mchezo huo,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Ally Manyani
alisema ushindi huo umewapa matumaini makubwa ya kuendelea kujipanga ili kuweza
kupata matokeo mazuri lengo likiwa kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Mwisho.
EmoticonEmoticon