NA SALMAH MUHIDINI,TANGA.
MWENYEKITI wa Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora amewataka
wapenzi na wanachama wa timu hiyo kuendeleza mshikamano lengo likiwa kupiga
hatua mbele za kimaendeleo kwenye mikakati waliojiwekea.
Aurora aliyasema hayo hivi
karibuni baada ya kufungua matawi mawili ya klabu hiyo moja likiitwa Saigon lililopo Mabanda ya Papa na Coastal Nyumba
lililopo katikati ya Jiji la Tanga ambapo jumla ya wanachama wapya 120
walipokelewa.
Alisema ni vema hasa kwenye kipindi hiki cha kuelekea
usajili wanachama na wapenzi wapaswa kuonyesha mshikamano na utulivu ili
viongozi waliopewa mamlaka waweze kufanya kazi hiyo kubwa iliyopo mbele yao lengo likiwa ni
kujiandaa vema na ligi kuu.
“Ndugu zangu
wanachama na wapenzi tusibaguane tuungane pamoja kwani tunajenga nyumba moja
kwanini tugombee fito, badala yake tuwe kitu kimoja kuhakikisha timu yetu
inapata maendeleo makubwa “Alisema Aurora.
Katika hatua nyengine,Mwenyekiti huyo alisema usajili wa
timu hiyo msimu huu utakuwa ni wa kihistoria kutokana na mikakati mizuri
waliojiwekea uongozi huo kuhakikisha wanasajili wachezaji wazuri watakaofanya
vizuri kwenye kikosi hicho cha wagosi wa kaya.
EmoticonEmoticon