Kocha
Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23
watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16
waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi
itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.
Wachezaji
walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Deogratias Munishi (Yanga) na
Mwadili Ali (Azam). Mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael
(Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan
Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba).
Washambuliaji
ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio
(Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC),
Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan
Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe,
DRC).
Wachezaji
walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko
Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram
Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba
(Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah
Sozigwa (Ilala).
Viungo
ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi),
Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona
(Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito
(Manyara).
Washambuliaji
ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati
(Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara
(Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga
Athanas Fabian (Mbeya).
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.
EmoticonEmoticon