MAMA SALMA APOKEA MBIO ZA PIKIPIKI KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUNGANO-ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI

April 18, 2014


 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara ndugu Mohamed Sinani  akikabidhi picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Mama Salma Kikwete na picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa Abeid Aman Karume kuashiria muendelezo wa mbio za uzalendo za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo.
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Said Sinani (mwenye kofia) akifuatana na viongozi wenzake wa Chama Cha Mapinduzi na Umoja wa Vijana kwenda kukabidhi mbio za pikipiki kwa uongozi wa Mkoa wa Lindi kwenye Kijiji cha Madangwa jana.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  wa Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini mtoto Idd Omar kutoka katika Kijiji cha Madangwa , kata ya Sudi huko Lindi Vijijini. Mama Salma alifika kijijini hapo kwa ajili ya kupokea mbio za uzalendo za pikipiki zilizoandaliwa na Umoja wa Vijana, (UVCCM) kitaifa zikitokea Mkoa wa Mtwara.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Madangwa namna ya kushika mfagio ili usiweze kuleta madhara kwa watoto waliobeba na hata wengine na pia ni njia bora ya kulinda afya zao kwani wakishika upande unaotumika kufagia wanaweza kupata magonjwa ya kuambukizwa.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Madangwa namna ya kushika mfagio ili usiweze kuleta madhara kwa watoto waliobeba na hata wengine na pia ni njia bora ya kulinda afya zao kwani wakishika upande unaotumika kufagia wanaweza kupata magonjwa ya kuambukizwa.
 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara ndugu Mohamed Sinani  akikabidhi picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa na picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa Abeid Aman Karume kwa Mama Salma Kikwete kuashiria muendelezo wa mbio za uzalendo za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar. KWA MATUKIO ZAID KATIKA PICHA BOFYA READ MORE

 Makabidhiano rasmi yakiendelea huku mamia ya wananchi  waliofurika kushuhudia wakishangilia.
 Baadhi ya Viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano.
 Bwana Salum Musa Mtungulu mkazi wa Kijiji cha Madangwa alitumia fursa hiyo ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kurejea Chama Cha Mapinduzi akitokea Chama Cha NCCR- Mageuzi. Katika picha hiyo anatoa maelezo  ya kitendo hicho huku makada wakimvisha mavazi ya Chama Cha Mapinduzi.
 Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM kutoka Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mnazi Mmoja kilichoko katika Kata ya Mingoyo walifurika kushuhudia sherehe za mbio za pikipiki za uzalendo kusherehekea miaka 50 ya Mungano .
Wasanii wa Kata ya Mingoyo wakitoa burudani wakati wa sherehe ya mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano zitakazofikia kilele Aprili 26.
 Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Madangwa na wageni waliohudhuria sherehe ya kupokea mbio za pikipiki kwa Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojumuisha Ruvuma, Mtwara na Lindi katika kusherehekea miaka 50 ya Mungano.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Seleman Salum Namputa, miezi 3, aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine. Kulia ni Mama mzazi wa mtoto Seleman ajulikanaye kama Mariam kutoka katika kijiji cha Moka huko Lindi Vijijini. Mama Salma alitembelea hopitalini hapo.
Mama Salma, akizungumza wakati wa mkutano huo. PICHA NA JOHN LUKUWI. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »