Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali,katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha Julai
hadi Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana jioni.
Baadhi
ya Viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakiwa katika kikao
cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi kwa kipindi cha robo mwaka kutoka
Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar
jana jioni, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.
*WAUMINI WA DINI YA KIKRISTU WAHUDHURIA IBADA MAALUM YA IJUMAA KUU LEO KANISA LA KKKT
Muumini
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika wa Azania
Front, Moses Kombe, (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu
ya Kuwambwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita wakati wa ibada ya Ijumaa
Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowasa akiwa katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la KKKT la Azania Front Dar es Salaam.
Waumini wa Kanisa la Kiinjili Tanzania KKT, la Azania Front la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph wakiwa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika leo kanisani hapo.
Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoriki,Mwadhama Porkap Kadinali Pengo
akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika
Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam leo.
Waumuni
wa Kanisa la Mtakatif Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa
wanaubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika jijini Dar
es Salaam leo.
Mtoto, Vanes Mpupua akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Mtakatif Josef Dar es Salaam.
Mmoja
wa Watoto waliofika katika Kanisa la Mtakatif Josef akiubusu Msaraba
wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliofanyika Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA
PHILEMON SOLOMON
*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI MJINI UNGUJA KUFUNGUA KONGAMANO LA MUUNGANO KESHO.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya maafisa na viongozi wakati alipowasili kwenye
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mjini Zanzibar leo jioni kwa ajili ya
kufungua rasmi Kongamano la Muungano, linaloanza kesho katika Ukumbi wa
Hoteli ya Zanzibar Beach Resort. Wa pili (kulia) ni mkewe Mama Zakia
Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya maafisa na viongozi wakati alipowasili kwenye
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mjini Zanzibar leo jioni kwa ajili ya
kufungua rasmi Kongamano la Muungano, linaloanza kesho katika Ukumbi wa
Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
EmoticonEmoticon