DC DENDEGO AWAFUNDA WAZAZI TANGA.

April 17, 2014
NA SALUMU MOHAMED,TANGA.
MKUU wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego amekemea vikali tabia ya baadhi ya wazazi wilayani hapa ambao huwaoza mabinti zao wakati bado wapo masomoni kwa kuwataka kuacha mara moja la sivyo watachukuliwa hatua kali zidi yao ili kukomesha vitendo hivyo kwenye jamii.

Aliyasema hayo  wakati wa mahafali ya 12 shule ya sekondari ya St.Christina iliyoko Kange Maziwa mjini hapa na kusema kuwa tabia ya wazazi kuwapa waume mabinti zao wakati wakiwa shuleni inasikitisha na hivyo ofisi yake imeadhimia kuikomesha.

Alisema kitendo hicho kinawanyima mabinti hao haki ya kupata elimu na kuweza kumkomboa mwanamke katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii hasa kwa wakati uliopo  sasa wa sayansi na teknolojia ulimwenguni.
Dendego alisema kupitia mahafali hayo wazazi na walezi ikiwemo wakina mama na wababa kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja ili kuweza kutokomeza vitendo vya wanafunzi wa kike kupewa wanaume wakati wakiwa masomoni.
“Nadhani hao wazazi wenye tabia hii kwa kweli  wako na jambo kama sio maslahi ni shida za papo kwa papo---sera ya mwanamke kuongoza na kuweza bila kuwezeshwa haijawafika baadhi ya wazazi na hivyo nawataka kuelimika” alisema Dendego
 

Alisema ofisi yake haitomvumilia mzazi wala mlezi yoyote atakaebainika kumuoza binti yake wakati yuko katika masomo na hivyo atahakikisha tabia hiyo inakomeshwa ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu na kuweza kuleta mapinduzi ya ukombozi wa wanawake katika kujiletea maendeleo.

Akizungumzia wazazi kuwabidiisha watoto wao katika elimu, Dendego aliwataka kuwa na ada ya kuwafuatilia maendeleo yao shuleni na kuacha kuwaruhusu kushiriki katika shughuli ambazo zinaweza kumtoa kimawazo katika masomo yake.
 

Alisema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatumia vibaya watoto vipindi vya likizo kwa kuwapa kazi ambazo ziko nje ya uwezo wao pamoja na kuwashirikisha katika biashara na kusahau kuwa vipindi hivyo ni vya maandalizi ya kujiandaa na masomo yalioko mbeleni kwao.
“Ni jambo la kushangaza kuona vipindi vya likizo kwa wanafunzi wazazi wanafurahia kama wamepata kitu kizuri---kumbe furaha yao ni kuwatumikisha katika kazi ambazo ziko nje ya uwezo wao na kusahau kuwa nihatari” alisema Dendego
Alisema ili kuwawezesha watoto kufanya vizuri vipindi vyote vya masomo yao ni jukumu la wazazi kuwabidiisha katika masomo vipindi vya likizo ili karo wanazolipa faida yake iweze kuonekana na kuacha kuzilaumu shule kuwa hazisomeshi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »