Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma na kupokewa na Mkuu wa Mkoa huo Dr. Rehema Nchimbi tarehe 11.4.2014. |
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwa shamrashamra za kwaya na matarumbeta wakati alipotua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ziara ya siku tatu mkoani humo.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipanda mti eneo la
jengo la utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati alipotembelea chuoni
hapo kwa ajili ya kufungua rasmi kongamano la Mustakabali wa mtoto wa
kike katika mazingira ya sasa kwa wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu
vilivyopo Dodoma na Morogoro. Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi
wa Chimwaga tarehe 12.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa ukumbini na wanafunzi wa kike waliojawa na furaha na hamasa kubwa
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza kwa nderemo na vifijo na
wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu mbalimbali vya Dodoma na Morogoro wimbo
uitwao ..”wanawake na maendeleo..” mara baada kuingia ukumbini. Mama
Salma alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kongamano la mustakabali wa
mtoto wa kike katika mazingira ya sasa.
Kaimu
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Herman Mlacha
akimkabidhi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete zawadi ya ramani ya Tanzania
yenye kuonyesha pia picha ya Chuo Kikuu cha Dodoma mara baada ya
ufunguzi wa kongamano hilo tarehe 12.4.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wanafunzi wa kike
kutoka vyuo vikuu waliofurika katika ukumbi wa Chimwaga huko Dodoma
tarehe 12.4.2014.
EmoticonEmoticon