\
Dar es Salaam. Michuano ya Kombe la Kagame imepangwa kufanyika nchini Tanzania mwanzoni mwa mwezi Juni huku Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) likiwa kwenye mazungumzo ya mwisho na wadhamini wa michuano hiyo.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye
alisema jana kuwa kesho Jumatatu wanatarajia kumtangaza mdhamini wa michuano hiyo kwenye ukumbi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kumalizana naye.
alisema jana kuwa kesho Jumatatu wanatarajia kumtangaza mdhamini wa michuano hiyo kwenye ukumbi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kumalizana naye.
“Tupo kwenye mazungumzo ya mwisho na wadhamini
wetu, nakuja huko Dar es Salaam kumalizana na wadhamini wetu, kila kitu
tutaweka wazi Jumatatu, ngoja kwanza tumalizane nao,”alisema Musonye.
Cecafa imekuwa ikihaha kusaka wadhamini wa kuandaa
michuano hiyo, ambapo awali walitangaza itafanyika Rwanda, lakini
Rwanda ikawatolea nje kubeba gharama hizo, ambapo Cecafa wameamua sasa
michuano ifanyike kwenye ardhi ya Tanzania.
Habari ambazo gazeti limezipata zinasema kuwa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lipo tayari kuisaidia Cecafa kubeba
michuano hiyo kwa kuziingiza timu nne za Tanzania bara ambazo ni Simba,
Yanga, Azam, na Mbeya City.
“Michuano hiyo inagharimu dola za Marekani 600,000
(Dola 1= Sh 1,594.90) na Cecafa haina kitu, TFF imezishauri iingize
timu nne za Tanzania bara kwa vile zina mashabiki kwani Mbeya City
ikicheza na Yanga au Simba zote zina mashabiki hivyo zitaingiza fedha za
kutosha kuendesha mashindano hayo,”alisema kiongozi mmoja ndani ya TFF.
Katika michuano ya mwaka jana ambayo ilifanyika
Darfur, Sudan, timu ya Vital ‘O’ ya Burundi ilinyakua ubingwa huku timu
za Tanzania zikiwa zimejitoa.
Hata hivyo, kutokana na ukata unaoikabili Cecafa
imebidi ikubali timu za Tanzania, Simba na Yanga kushiriki kwani
zilijitoa kwenye michuano hiyo mwaka jana kutokana na kuzuiwa na
Serikali kwa kile kilichoelezwa kuwa hali ya usalama katika miji ya El-
Fasher na Kadugli huko Darfur siyo nzuri na kuzikataza timu za Simba na
Yanga kwenda kushiriki michuano hiyo inayodhaminiwa na Rais wa Rwanda,
Paul Kagame kwa jumla ya dola za Marekani 60,000.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI
EmoticonEmoticon