NA SAFARI CHUWA,TANGA.
Bao la Gido Chawala lililofungwa dakika ya 17 lilitosha
kuwapa ushindi Jkt Ruvu kwenye mechi yao ya Ligi
kuu ya Vodacom Tanzania
dhidi ya Coastal Union ya Tanga mchezo uliochezwa kwenye dimba la CCM Mkwakwani
hii leo.
Bao hilo lilitokana na penati
iliyotolewa na mwamuzi wa mchezo huo Adrew Sahmba kutoka mkoani Pwani kuamuru
ipigwe kutokana na mshambuliaji wa Coastal Union,Selemani
Kassim Selembe kuunawa mpira eneo la hatari.
Hata hivyo baada ya kuingia bao hilo,Coastal Union
walijitahidi kupambana kufa na kupona ili kutaka kulirudisha bao hilo bila
mafanikio ya aina yoyote yale ambapo pia Mchezo huo ambao ulikuwa wa kawaida
kwa timu zote kucheza na kushambuliana kwa zamu.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kufanya
mabadiliko ambapo Coastal Union iliwatoa Sulemain Kassim Selembe,Mohamed Ally
na Hamadi Juma na kuwaingiza Mohamed Soud,Yayo Lutimba na Rayzin Haji ambao
kuingia kwao kuliweza kuongeza nguvu licha ya kutokuweza kubadili matokeo.
Mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yaliweza kusomeka kuwa
Coastal Union 0,JKT Ruvu 1.
Jkt Ruvu leo iliwakilishwa na Shabani Dihile,Damas
Makwaya, Edward Charles,Chacha marwa,kasimba luambano,Thomas ndimbo, haruna
adolf,paul ndauka,samweli kamutu na gido chawala,.
Coastal union iliwakilishwa na Fikirini bakari,hamadi
juma,abdi banda,yusuph chuma,mbwana bakari,razack khalfani,Mohamed ally,ally
iddi,Mohamed mtindi,Mohamed rajabu na suleiman kassim selembe.