Rais
Jakaya Kikwete leo ameongozi taifa katika maadhimisho ya miaka 30 ya
kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Edward Moringe Sokoine katika maadhimisho
yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu Monduli Juu.
Pichani ni juu Rais
Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa
Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa kumbukumbu ya miaka 30 tangu kifo
chake.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa akiweka shada la maua
katika Kaburi la marehemu, Edward Moringe Sokoine.
Spika wa Bunge Anne Makinda akiweka shada la maua.
Mjumbe wa Bunge la Katiba Paul Kimiti akiweka shada la maua kwaniaba ya wajumbe wenzake.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishiriki misa
maalum ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania
Hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika nyumbani kwake Monduli. Kulia kwake
ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenera Mkungara, na
motto wa Marehemu sokoine Ndugu Joseph Sokoine
Viongozi mbalimbali wakishiriki katika Misa maalum ya kumuombea Marehemu.
Rais Kikwete akisalimiana na Spika wa Bunge Anne Makinda.
Rais
Kikwete, akiwa katikati ya wajane wa waziri Mkuu wa Zamani Edward
Moringe Sokoine wakati wa kumbukumbu ya Kiongozi huyo wa zamani wa
Tanzania. Wengine kutokla kushoto ni Mjane wa baba wa Taifa, mama Maria
Nyerere, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Spika wa Bunge, Anne Makinda
namotto wa Marehemu sokoine Ndugu Joseph Sokoine.
EmoticonEmoticon