*KAMATI ZAANZA KUWASILISHA TAARIFA ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA, WENGI WAPENDEKEZA SERIKALI MBILI

April 10, 2014

 Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Bunge hilo leo mjini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa Sura ya Kwanza na Sita wa rasimu ya Katiba mpya.
 Makamu  Mwenyekiti wa Kamati namba tano Assumpter Mshama akiwasilisha maoni ya wajumbe wa Kamati yake leo mjini Dodoma juu ya uchambuzi wa sura ya kwanza na sita ya wa rasimu ya Katiba mpya.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya kusilikiliza uwasilishaji wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya.Picha na Bunge Maalum la Katiba.
***************************************
Na Magreth Kinabo- Dodoma
Baadhi ya Kamati 12 za Bunge Maalum la Katiba leo zimeanza kuwasilisha  taarifa zao  kuhusu  sura ya kwanza nay a sita ya Rasimu  ya Katiba  ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania katika Bunge hilo, mjini Dodoma, huku maoni ya walio wengi wapendekeza Serikali Mbili.

 Uwasilishaji wa taarifa hizo ulianza mapema leo asubuhi mara baada ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kuanza kikao, ambapo Kamati mbili ndizo zilizopata fursa ya kuwasilisha, kwa mujibu wa muda uliopangwa .Kamati nyingine zitaendelea  sasa 10: 00 jioni.

 Kamati iliyokuwa ya kwanza kuwasilisha taarifa  hiyo ni Kamati namba mbili, ambayo Mwenyekiti wake ni Shamsi Vuai Nahodha , ambaye ndiye aliyeiwasilisha katika Bunge hilo.

Akiwasilisha taarifa hiyo, Nahodha, aliliarifu Bunge hilo, kuwa zipo baadhi ya ibara ambazo hakikuungwa mkono kwa theluthi mbili kwa mujibu wa Kanuni ya 64(1) ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba za mwaka 2014.

Alizitaja ibara  hizo ni ibara ya inayohusu “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, ibara inayohusu “Ukuu na Utii kwa Katiba,” ibara ya 60 inayohusu “Muundo wa Muungano “na  ibara ya 61 inayohusu” Vyombo vya Utendaji vya Jamhuri ya Muungano”.

 "Kutokana na hali hiyo na kwa kuzingatia kanuni niliyoitaja hapo awali, ibara hizi zinachukuliwa kuwa zimefanyiwa maamuzi, lakini hazikupata theluthi mbili ya upande mmoja. Kwa msingi  huo Kamati yangu inazileta ibara hizo pamoja na ibara nyingine mbele ya Bunge hili Maalum ili kufanyiwa maamuzi ya pamoja,” alisema Nahodha.

 Akiwakilisha maoni ya walio wengi  kuhusu sura ya kwanza ibara ya kwanza(i)inayohusu “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”    alisema wajumbe walikuwa na mjadala maana na maneno  ya “Muungano na “Shirikisho”.  Hata hivyo  katika mjadala huo ufafanuzi   kina ulitolewa kuhusu maneno hayo.

 Alisema neno Muungano ni makubaliano  ya zaidi ya nchi moja kuunda dola moja yenye nguvu ambapo majukumu ya msingi ya nchi hizo yanakabidhiwa kwenye Serikali ya Muungano, wakati Shirikisho ni makubaliano ya nchi mbili au zaidi zinazounda Serikali moja chini ya kiongozi mmoja.

 Hivyo  baada ya  ufafanuzi huo wajumbe walifanya maamuzi katika ibara ya kwanza(1)wajumbe wengi walipendekeza neno shirikisho lifutwe kwa sababu tatu, ambazo  kwanza  ni hati ya makubaliano ya Muungano inazungumzia kuwepo kwa Serikali mbili yaani Serikali ya Muungano na Serikali ya mapinduzi  ya Zanzibar. Hata Rasimu ya Katiba ibara 1(3) inatambua  hati ya Muungano kama msingi na muendelezo wa makubaliano hayo.

Pili hati  hiyo ya Muungano mpaka sasa bado haijafutwa na wala haijabadilishwa na tatu Shrikisho la serikali tatu linalopendekezwa katika rasimu , litakuwa dhaifu kiasi cha kushindwa kudhibiti ulinzi wa eneo la bahari ya Hindi lenye rasilimali nyingi ambazo mataifa makubwa wanaziwania.

Aliongeza kuwa udhaifu huo utayapa mwanya mataifa hayo kuzirubuni nchi washirika zisichangie gharama za kuendesha Serikali ya  Shirikisho, hasa kwa kuzingatia kuwa Serikali Shirikisho haina vyanzo   vya uhakika vya  mapato  ,hivy endapo jambo hilo likitokea Shirikisho litadhoofika na hatimaye kuvujika.

Aliongeza kuwa katika sura ya sita ibaraya 60 kuhusu  Muundo wa Jamhuri ta Muungano wajumbe wengi walikubaliana kuwa Muundo wa Serikali Mbili kama ilivyoanishwa katika hati ya Muungano wa Tanzania, baada ya kupiga kura kwa ajili ya kupata uamuzi ,theluthi mbili upande wa Tanzania Bara haikupatikana. 

Hata hivyo wajumbe wengi walipendekeza ibara hiyo ifanyiwe marekebisho kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na Serikali mbili ambazo ni  Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar. 
                 
Nahodha alisema kwa maoni ya watu wachache , katika sura ya kwanza 1(1) walipendekeza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka kamili limetokana na Muungano wa Nchi huru  mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Aidha aliongeza kuwa katika sura ya sita, ibara, 60 hadi 69 zinahusu Muundo wa Serikali walipendekeza zibaki na zisomeke kama zilivyo katika rasimu.

Kwa upande wake  Makamu  Mwenyekiti wa Kamati namba tano (5)ya Bunge hilo, Assumpter Mshama  ambayo ilikuwa ya pili kuwasilisha ripoti yake , alisema  ibara ya kwanza(1)  haikupata theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka Tanzania Bara,lakini ilipata theluthi mbili  ya wajumbe kutoka Zanzibar.

 Aliongeza kuwa ibara ndogo ya (2) na (3) zilipata theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

 Hivyo wajumbe walio wengi kwa kuzingatia Hati ya Makubaliano walipendekeza mfumo wa Serikali Mbili ndiyo unaofaa, ndiyo utakaoimarisha Muungano kama changamoto zilizobainishwa zitatuliwa kisheria na kikatiba.

 Assumpter   alisema katika sura sita ibara ya 60 ilikataliwa na theluthi mbili ya  wajumbe kutoka Tanzania Bara na  Zanzibar. Hivyo walipendekeza  ibara ya 60 (1) itakuwa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa Serikali mbili, ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Alisema  maoni ya walio wachache  sura ya kwanza ibara ndogo ya kwanza  wajumbe walipendekeza kuwa ibaki kama ilivyo lakini irekebishwe kidogo, isomeke Shirikisho la Jamhuri ya Tanzania, ni Shirikisho ambalo limetokana na Muungano wa Nchi mbili za Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

ibara 1(4) Nchi nyingine yoyote ya Afrika itaweza kujiunga na Shirikisho ili  mradi  tu inakubaliana na masharti ya Katiba  hii.”

Alisema  sababu walizozitaja ni  Muungano wa Tanzania umetokana na Jamhuri ya mbili kuungana kwa hiari, jina la awali  lililotajwa katika Mkataba wa Muungano lilikuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tangayika na Zanzibar.Jina hili lilibailishwa na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Katika taarifa za kamati hizo, baadhi ya ibara zilifanyiwa marekebisho na nyingine zibaki kama zilivyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »