WAMA YAZUNGUMZIA MAHUSIANO MEMA KATI YAO NA JAMHURI YA WATU WA CHINA

April 10, 2014


 Mkurugenzi wa Uboreshaji Afya Wama ,Dkt.Sarah Maongezi (Kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu ushirikiano uliopo  baina ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo pamoja na Jamuhuri ya Watu wa China nchini katika kusaidia wananchi ikiwemo ziara wanaoyotarajia kuifanya katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuanzia tarehe 12 hadi 19 Aprili mwaka huu,Katika ni katibu wa Balozi wa China nchini,Ren Zhihong na Meneja Mawasiliano wa Wama Philomema Marijani.
Katibu wa  Balozi wa Jamuhuri ya watu wa China nchini, Ren Zhihong (katika) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano uliofanyika maelezo leo jijini Dar es salaam kuelezea ushirikiano uliopo baina ya Taasisi ya Wama na Ubalozi wa China katika shughuli za kusaidia jamii.Kulia ni Mkurugenzi wa Uboreshaji Afya Wama ,Dkt.Sarah Maongezi na kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Wama Philomema Marijani.

Picha na Lorietha Laurence
******************************************
Na Lorietha Laurence
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo  kwa kushirikiana na Balozi wa Jamuhuri  ya watu wa china nchini,  Lu YouQing  itafanya ziara kuitembelea mikoa ya kanda ya ziwa kuanzia tarehe 12 hadi 19 Aprili mwaka huu kwa  shughuli za kusaidia jamii.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Uboreshaji Afya ,Dkt.Sarah Maongezi   amesema lengo la ziara hiyo ni kusaidia jamii za watu wa kanda ya ziwa katika sekta za afya.elimu pamoja na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi.

“Lengo kuu la ziara hii ni kuwasaidia wananchi wa mikoa ya Mara,Simiyu,kagera na kigoma kwa kutoa huduma ya afya na elimu bure pamoja na kuwasaidia wanawake waweze kujiinua kiuchumi  ili kuimarisha ushirikiano wa shughuli za maendeleo na uwekezaji”alisema Dkt.Maongezi.

Aliongeza kuwa shughuli zitakazofanywa katika ziara hiyo ni kuwatambulisha  wataalamu wa afya kutoka china ambao watatoa huduma ya upimaji wa afya na dawa  bure katika hospitali ya wilaya ya Butima,na  msaada ya vyerehani kwa vikundi vya wanawake wajisiriamali pamoja na vitabu,mabegi  na mipira ya kuchezea. 

“Wama haiko kwa ajili ya wanawake na watoto wa kike tu bali inasaidia watu wote wake kwa waume,kwasababu  kila alipo mwanamke na mwanaume naye yupo nyuma yake hivyo inawahusisha watu wote ingawa imejikita zaidi kwa wanawake.”alisema Dkt. Maongezi.

Naye katibu wa Balozi wa Jamuhuri ya watu wa china nchini Ren Zhihong ameusifu uhusiano mzuri uliojengeka kati ya serikali ya Jamuhuri ya watu wa china na Tanzania ilidumu kwa miaka 50, na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo katika k shughuri mbalimbali za kijamii.

Taasisi ya Wama  ipo chini ya uongozi wa Mhe. Mama Salma Kikwete na imejidhatiti katika kuwawezesha wanawake na wasichana ili kujenga jamii yenye afya,maendeleo na iliyoelimika, ikisimamia dira ya “Wanawake wa Tanzania wanawezeshwa kuishi maisha bora”.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »