April 09, 2014

MVUA YAAHIRISHA MECHI YA AZAM NA RUVU SHOOTING

Na Mahmoud Zubeiry, Mlandizi

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Ruvu Shooting na Azam FC ya Dar es Salaam uliokuwa ufanyike jioni ya leo Uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani umeahirishwa hadi kesho kufuatia mvua kubwa.
Timu hazikuwahi hata kuingia uwanjani kupasha misuli moto kutokana na mvua kubwa na Uwanja kujaa maji na ilipowadia Saa 10:20 waamuzi wa mechi hiyo waliingia uwanjani kukagua na kuvunja mchezo.

Hii ndiyo hali ya Uwanja wa Mabatini leo hadi mchezo baina ya Azam na Ruvu ukaahirishwa

Kilifuatia kikao cha pande zote nne, baina ya viongozi wa Ruvu na Azam pamoja na TFF na marefa ambao waliafikiana mechi ichezwe kesho iwapo hali itakuwa nzuri.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alikuwepo na kushuhudia hali hiyo.
Isihaka Shirikisiho wa Tanga ndiye aliyetarajiwa kuwa refa wa mchezo wa leo, akisaidiwa na Hassan Zani na Agness Pantaleo wote wa Arusha na refa wa akiba mwenyeji, Simon Mbelwa.
Waamuzi wakikanyaga maji uwanjani wakati wa ukaguzi
Marefa wakijiandaa kuahirisha mchezo

Azam yenye pointi 53 itaendelea kuishi kileleni mwa Ligi hata Yanga SC inayocheza na Kagera Sugar hivi sasa mjini Dar es Salaam itashinda, kwani wana Jangwani hao watatimiza pointi 52 huku pia wakiwa wamecheza mechi moja zaidi

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »