TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YATETA NA WANAHABARI DAR
Katibu
Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Adam Mambi akiwaeleza
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa kuanza utafiti
katika mapitio ya mfumo wa sheria unaosimamia haki za walaji ikiwa ni hatua
mojawapo katika mchakato wa kuundaa
sheria inayowalinda watumiaji wa huduma mbalimbali hapa nchini. Kulia ni
Afisa Sheria wa Tume hiyo ni Fred Kandonga.
Afisa
Sheria wa wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Fred Kandonga akijibu maswali
ya waandishi wa habari kuhusu sababu zilizopelekea Serikali kuamua kufanya
utafiti utakaopelekea kutungwa kwa sheria itakayosaidia kuwepo kwa mfumo nwa
biashara wenye uwiano katika ushindani. Katikati ni Katibu Msaidizi wa Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Adam Mambi, anayemfuatia ni Afisa Habari Idara
ya Habari Maelezo Frank Mvungi na Mwisho kushoto ni Afisa habari wa Tume hiyo
Munir Shemweta.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TUME YAANZA UTAFITI KATIKA MAPITIO YA MFUMO WA SHERIA
UNAOSIMAMIA HAKI ZA WALAJI
Tume
ya Kurekebisha Sheria Tanzania imeanza kufanya utafiti wa mfumo wa
sheria unaosimamia Haki za Walaji ili kubaini kasoro mbalimbali
zilizoko kwenye mfumo husika na
kupendekeza njia sahihi ya kuboresha mfumo huo nchini Tanzania.
Hatua ya Tume kufanya utafiti huo inatokana na mendeleo ya sayansi, teknolojia
pamoja na utandawazi ambayo kwa ujumla yamemfanya mlaji kujikuta akiwa kwenye
hatari ya kuathirika kiafya, kiuchumi na kijamii.
Tume katika utafiti wa awali, imebaini kuwa Mfumo uliopo hauendani
na na wakati huu wa mabadiliko ya
kiuchumi, kijsamii, kitekenologia yanayotokea, kwani sheria nyingi zilizopo
zilitungwa muda mrefu na hivyo hazikuzingatia mahitaji ya wakati wa sasa.
Pia sheria nyingi hazijajumuishwa
kwenye sheria moja zinasimamiwa na watu
au Taasisi tofauti tofauti. Hivyo, Tume imeona haja ya kupitia sheria hizo ili
kupendekeza mfumo wa sheria utakaomlinda
mlaji kwa kuzingatia maendeleo yaliyopo sasa.
Na ni matarajio
yetu baada ya kukamilika kwa utafiti huu Tume tutakuja na mapendekezo ambayo
yataleta tija kwa walaji wetu pamoja na taifa kwa ujumla.
Tume ya Kurekebisha Sheria
(Tume) ilianzishwa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Kurekebisha Sheria
Namba 11 ya mwaka 1980. Sheria hii kwa sasa ni Sura ya 171 ya Sheria za
Tanzania Toleo la Mwaka 2002. Tume ya Kurekebisha Sheria ni Idara ya Serikali
inayojitegemea chini ya Wizara ya Katiba
na Sheria.
Imetolewa
na;
Tume ya
Kurekebisha Sheria (T)
Dar es
Salaam
04 Aprili,
2014
EmoticonEmoticon