March 30, 2014

VPL:YANGA SC YAPINGWA 2-1 MKWAKWANI AZAM FC AILAMBA SIMBA 2-1


Jumamosi Machi 29
Ashanti United 2 JKT Oljoro 1
Jumapili Machi 30
Azam FC 2 Simba 1
Mgambo JKT 2 Yanga 1
Mbeya City 1 Tanzania Prisons 0
Kagera Sugar 0 v Ruvu Shooting 0
Mtibwa Sugar 3 v Coastal Union 1
JKT Ruvu 3 v Rhino Rangers 1
MABINGWA Watetezi Yanga Leo huko katika dimba la Mkwakwani Tanga walifungwa Bao 2-1 na Mgambo JKT iliyokuwa ikicheza Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Mohamed Neto kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 30 kwa kile kilichodaiwa kukutwa na Hirizi na kipigo hicho inaelekea kinapeleka Ubingwa kwa Azam FC ambao Leo wameichapa Simba Bao 2-1.
Huko Mkwakwani, Mgambo JKT walipata Bao lao la Kwanza Dakika ya Kwanza tu Mfungaji akiwa Fully Maganga na Yanga kusawazisha katika Dakika ya 50 kwa Penati ya Nadir Haroub "Cannavaro" lakini Penati nyingine iliyopigwa na Malima Busungu katika Dakika ya 69 iliwapa ushindi Mgambo JKT.
Jijini Dar es Salaam, Azam FC waliichapa Simba Bao 2-1 kwa Bao za Hamisi Mcha, Dakika ya 16, na John Bocco, Dakika ya 56 wakati Bao la Simba lilifungwa na Joseph Owino katika Dakika ya 45.
Matokeo haya yanaifanya Azam FC izidi kupaa kileleni wakiwa na Pointi 53 kwa Mechi 23 na kubakiza Mechi 3 huku Yanga wakiwa Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 46 kwa Mechi 22 na kubakisha Mechi 4.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »