NGUMI ZA NELSON MANDELA OPEN CHAMPIONSHIP ZAFUNGULIWA KAWE LEO.
Bondia Part Kimweri kutoka Tanga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Saidi Jabir wa Ngome Dar wakati wa mashindano ya wazi ya Nelson Mandela yaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam, Kimweri alishinda mpambano huo kwa pointi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com |
Baadhi ya viongozi wakifatilia mashindano hayo |
Marefarii , mabondia na Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya ufunguzi wa mashindano hayo. |
Mjumbe wa bft Antony Mwangonda akiwa na makamu wa rais Lukelo Willilo |
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya mchezo wa Ngumi yanayokwenda kwa jina la Nelsoni Mandela Open ChampionShip yameanza kutimua vumbi katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam
Akizungumzia mashindano hayo yalivyo na ubora wa ali ya juu Makamu wa Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa nchini 'BFT' Lukelo
Willilo 'amesema mashindano hayo kwa sasa yameboleshwa kwa kufuata
taratibu za chama cha ngumi za ridhaa Dunia kwa sasa mabondia awavai
kofia ngumu wanakuwa vichwa wazi hivyo wapenzi wa ngumi weje waone
mabadiliko makubwa katika ngumi za ridhaa ndio ambazo ni msingi wa
maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini;'
Zamani mabondia walikuwa wanavaa kofia lakini kutokana na mabadiliko
sasa awavai kofia wanapigana vichwa wazi ambapo kwa kuanzia tumeamua
kuweka mashindano haya kwenye viwanja vya wazi na ni bule tu akuna
kingilio ili kila mtu ajionee mabadiliko ya ngumi mashindano hayo yanayo
husisha mikoa mbalimbali nchini
Mashindano haya yatakuwa ya siku tano kuanzia jumatano mpaka jumapili na
ngumi zinanza kupigwa saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku ngumi ndio
zitakuwa zikisha
Katika
ufunguzi huo bondia Patrck Kimweri wa Tanga alishindwa kufurukuta mbele
ya Said Jabir wa ngome na Rashidi Samvu wa Kigoma alipigwa kwa pointi
na Hafidhi Kassimu wakati Fabian Gaudence akimsambalatisha Hussein Mnimbo