Release No. 017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 3, 2014
TFF
YAADHIMISHA MIAKA 50 FIFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaadhimisha miaka 50 tangu lipate uanachama
wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) kwa shughuli mbalimbili
ikiwemo michezo na makongamano.
Kamati
maalumu itaundwa kwa ajili ya kupanga na kuratibu shughuli hiyo ambayo TFF
imepanga kuadhimisha nchini nzima kwa kutumia wanachama wake.
TFF
wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) ilijiunga na FIFA
Oktoba 8, 1964.
PAMBANO LA
YANGA, MBEYA CITY LAINGIZA MIL 175
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Yanga na Mbeya City lililofanyika
jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh.
175,285,000.
Watazamaji
30,411 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio sh. 5,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Yanga ndiyo iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mgawanyo
wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama
za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50.
Uwanja
sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh. 13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,096,959.36.
Nayo
mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000 ambapo kila timu imepata sh.
11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267.
Mgawanyo
mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 4-0 ni Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 7,277,033.90 na gharama za kuchapa tiketi sh.
2,278,400.
Uwanja
sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh. 3,433,460.95, Bodi ya Ligi sh. 3,433,460.95,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,716,730.47 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,335,234.81.
TFF YAPATA
HATI YA KIWANJA TANGA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepata hati ya kiwanja chake kilichopo eneo
la Mnyanjani katika Jiji la Tanga.
Hati
hiyo ya miaka 99 ya kiwanja hicho namba 75 Block D chenye ukubwa wa ekari 7.6
ilikabidhiwa kwa TFF, Januari 13 mwaka huu.
Kiwanja
hicho kitaendelezwa kwa matumizi mbalimbali, kubwa ikiwa ni uwanja wa mpira wa
miguu.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
EmoticonEmoticon