MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA UKUMBI WA MIKUTANO WA KANISA LA MTAKATIFU PETER.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na waumini wa dini ya Kikristu wakati wa Ibada maalum ya
Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la
Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati
alipowasili kwenye Kanisa la Mtakatifu Peter Oysterbay, leo asubuhi kwa
ajili ya kushiriki katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa
mikutano wa Kanisa hilo. ambapo zaidi ya Sh. milioni 65 zilipatikana
kati ya Sh. milioni 600, zinazohitajika hadi ifikapo mwezi Julai. Kati
ya hizo Cash ni Sh. milioni 5 na zilizobakia zikiwa ni ahadi.
***************************************
Zaidi
ya shilingi milioni 65 zimekusanywa katika harambee iliyoongozwa na Makamu wa
Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa
mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililoko jijini Dar es salaam.
Kati
ya fedha hizo zilizokusanywa katika ibada maalum ya kuchangia ujenzi wa jengo
la ukumbi huo ilyoongozwa na Mhadhama Kadinali Polycap Pengo kiasi cha shilingi
milioni 60.5 zilikuwa ni ahadi na shilingi milioni 5 zikiwa ni fedha taslimu.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Makamu wa Rais aliwahakikishia Watanzania kuwa serikali
itaendelea kuunga mkono juhudi za taasisi za kidini katika kudumisha amani na
upendo ndani ya jamii bila ya kujali tofauti za aina yo yote ile.
Alisema
kuwepo kwake katika hafla hiyo ni ishara ya uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi mbali mbali za dini nchini.
“Sisi
Watanzania tumefika hapa kutokana na uongozi thabiti wa waasisi wa Taifa letu. Hivyo,
tunataka nchi ya watu wanaomwogopa Mungu, watu wanaopendana, watu
wanaovumiliana na watu wanaotakiana mema katika shughuli zao.”
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Bibi Rose Rupia kamati yake inahitaji
shilingi milioni 600 zaidi kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi wa jengo la
ukumbi huo na kwamba tayari wameshatumia kiasi cha shilingi bilioni moja katika
ujenzi huo.
Ibada
hiyo maalum ilihudhuriwa pia na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu wa
Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mwadhama Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada
maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa
la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akisalimiana na Mwadhama
Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia
ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo
Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akiongoza na na
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kutoka kanisani baada ya ibada hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter,
Stephano Kaombe, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa
Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam,
wakati wa harambee ya kuchangia ujnenzi wa Ukumbi huo iliyofanyika leo
asubuhi.
Picha ya pamoja......
Akitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa wakati
alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa
Kanisa la Mtakatifu Peter, baada ya ibada maalum ya harambee ya
kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika leo asubuhi, Jan 26, 2014. Kushoto ni
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe.
Chanzo Suffianimafoto.com