
Rais
mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiapishwa rasmi rais wa
nchi hiyo mjini Antananarivo kufuatia ushindi mkubwa alioupata katika
uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013.

Rais
mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akisani kiapo chake tayari
kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa Madagascar mbele ya Jaji Mkuu wan
chi hiyo Jean –Michael Rasolonjatovo (kushoto) wakati wa sherehe za
kumuapisha rais huyo zilizofanyika mjini Antananarivo.

Rais
mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akizungumza na wananchi wa
Madagascar waliofurika ndani ya uwanja wa Antananarivo mara baada ya
kuapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo mjini.

Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe
akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumuapisha rais
mpya wa Madagascar akiwa kwenye jukwaa kuu pamoja na viongozi wengine wa
nchi za Afrika waliohudhuria sherehe hizo mjini Antananarivo.Wengine
wanaoonekana kutoka kulia ni Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano,
Rais wa Zambia Ipikefunye Pohamba na aliyekuwa rais wa Madagascar Andry
Raojolina.

Gwaride maalum la jeshi la Madagascar wakati wa sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Hery Rajaonarimampianina.

Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akikagua gwaride la majeshi ya Madagascar baada ya kuapishwa.

Viongozi
mbalimbali na wanachi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya
wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina mjini Antananarivo.

Sehemu wa Umati mkubwa wa wananchi uliyoudhuria sherehe hizo

Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiwasili Ikulu ya nchi hiyo mjini Antananarivo.
----
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atamwakilisha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye sherehe
za kumwapisha Rais Mteule wa Madagascar, Mhe. Henry Rajaonarimampianina
zitakazofanyika nchini humo tarehe 25 Januari, 2014.
Mhe. Membe ataondoka
kwenda Madagascar tarehe 24 Januari, 2014. Mahakama Maalum ya Uchaguzi nchini
Madagascar ilimtangaza Mhe. Rajaonarimampianina kuwa mshindi wa uchaguzi wa
Urais tarehe 17 Januari, 2014.
Duru ya kwanza ya
uchaguzi huo ilifanyika tarehe 31 Julai, 2013, ambapo hakupatikana mshindi. Katika
duru ya pili iliyofanyika tarehe 20 Desemba, 2013, Mahakama Maalum ya Uchaguzi
ilitangaza kuwa Mhe. Rajaonarimampianina alipata asilimia
53.49 ya kura zote zilizopigwa huku mpinzani wake Bw. Jean Louis Robinson akipata
asilimia 46.51.
Kwa
kushirikiana na wanachama
wengine wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
Tanzania, ambayo ilikuwa mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na
Usalama ya SADC kwa mwaka
mmoja ulioishia Agosti, 2013, ilitoa mchango mkubwa kuhakikisha
Madagascar
inaendesha uchaguzi wake katika hali ya amani na utulivu na kwa
kuzingatia
misingi ya demokrasia, ili kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioibuka mwaka
2008
baada ya Bw. Andry Rajoelina kuingia madarakani kwa kusaidiwa na Jeshi.
IMETOLEWA
NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR
ES SALAAM
23 JANUARI, 2014,
Januari 23, 2014
EmoticonEmoticon