CHADEMA YAPATA PIGO TANGA,MWENYEKITI WA KATA WAO ARUDI CCM.

January 15, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kata ya Mwanzange jijini Tanga,Said Bakari amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuchoshwa na sera zisizotekelezeka ndani ya chama chake ambazo hazina mashiko.

Uamuzi huo aliutangaza katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata hiyo ulikuwa ukihutubiwa na Mwenyekiti wa cha Mapinduzi wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni ambao aliambatana na viongozi wengine wa chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kati kwenye mkutano huo,Bakari alisema awali alijiunga na chadema akitokea chama cha mapinduzi akidhani  chama hicho kina mashiko na wananchi badala yake mambo aliyoyakuta hayakuwa kama alivyotarajia.


Alisema hasa kikubwa kilichomfanya kukirudia chama hicho ni kutokana na utendaji makini unaofanywa na viongozi wa chama hicho ambao umepeleka kuweza kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali za wananchi.

Katika mkutano huo wanachama wengine waliojiunga na chama hicho waliweza kufikia idadi ya wanachama 111 ambao walikabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa CCM wilaya na baadae kula kiapo cha pamoja.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kadi hiyo kwa wanachama hao wapya,Mbughuni alisema chama hicho kitaendelea kujiimarisha lengo likiwa kuhakikisha wanaendelea kushika hatamu ya uongozi kwenye chaguzi zijazo wilayani hapa.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga(UVCCM) Salim Perembo aliwataka vijana kubadilika na kuacha kukaa vijiweni badala yake waunde vikundi vya ujasiriamali vitakavyoweza kuwakwamua kimaisha.

   "Vijana tusiwekeze akili zetu kwenye starehe badala yake tubuni
miradi ambayo inatuwezesha kuinua maisha yetu pamoja na jamii nzima inayotuzuguka "Alisema Perembo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »