WAHAMIAJI HARAMU 590 WAKAMATWA MKOANI TANGA.

January 01, 2014


Na Oscar Assenga, Tanga.
JUMLA ya wahamiaji haramu 590 walikamatwa mkoani Tanga katika kipindi cha  kuanzia Januari 2012 hadi octoba 2013 kutokana sababu mbalimbali ikiwemo kuingia nchini bila kibali na kufanya kazi.

Takwimu hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya mkoa wa Tanga mwaka 2012 hadi Octoba 2013 kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki.


Gallawa alisema kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2012 jumla ya watuhumiwa 289 wa mataifa ya Ethiopia 116,Kenya 53,Uganda 29,Switzerland 1,India 6,Italia 1,German 4,Afrika Kusini 3,Somalia 18,Portugues 1,Bangladesh 2,Denmark 1,Zambia 2,China 2,Congo1.

Aidha aliongeza kuwa wahamiaji haramu waliokamatwa kutoka mataifa mengine ni Guinea 1,Turkey 1,Sri-Lanka 1,Pakistan 6,Peru  1,Egypt 1,Norway 2 na watanzania 32 ambao walikamatwa kwa makosa yaliyotajwa hapo juu ukilinganisha na kipindi cha kuanzia Januari hadi Octoba 2013 ambapo jumla ya watuhumiwa  301 kutoka nchi mbalimbali waliokamatwa.

Gallawa alisema katika kipindi hicho wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia 213,Kenya 29,India 9,China 3,Bangladesh 7,Djibout 1,Pakistan 1,Burundi 1,Somalia 2,British 2,Osterech 1,Uganda 2,Israel 2,USA 2 na watanzania 25.

Aliongeza kuwa takwimu hizo zinaonyesha idadi ya wahamiaji haramu hasa raia wa Ethiopia waliokamatwa imeongezeka kati ya mwaka 2012 hadi kufikia Octoba 2013 .

Mkuu huyo wa mkoa alisema idadi ya watanzania waliokamatwa kwa kosa la kusaidia au kuwahifadhi na kuwasafirisha wahamiaji haramu imepungua ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2012.

Alisema takwimu hizo ni mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa idara ya uhamiaji Tanga kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari zitokanazo na wahamiaji haramu na ushirikishwaji wa wananchi dhidi ya mapambano ya kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu nchini.

Hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahamiaj haramu hao ni kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa nchini kwa kupewa notisi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »