MHARIRI WA MICHEZO WA GAZETI LA MTANZANIA, MWANI NYANGASSA, AONGOZA TEAM MAUZO YA NEW HABARI (2006) LTD KUSAMBAZA GAZETI HILO LILILOFUNGULIWA DESEMBA 27.

December 28, 2013
KUFUATIA kufunguliwa kwa Gazeti Bingwa la Habari Tanzania, MTANZANIA, linalochapishwa na Kampuni ya NewHabari (2006) LTD, Waandishi, Wahariri pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni hiyo leo walinaswa na Kamera yetu wakisambazas gazeti hilo katika Mitaa ya Dar es salaam.

Mpiga picha katika pita pita zake alikutana na Mhariri wa Michezo wa Gazeti hilo, lililotoka kifungoni leo, Mwani Nyangassa akiwa na nakala zake mkononi, katika juhudi za kulitangazia umma ujio mpya wa gazeti hilo.

Tizama katika picha matukio katika kilichojiri leo katika mitaa ya Sinza, Morroco, Kariakoo, Ubungo na maeneo mengine ya Jiji la Dar es salaam.
Mwani Nyangassa akifanya mauzo katika mitaa ya Jiji la Dar es salaam
Mhariri wa Michezo wa gazeti la Mtanzania, lililotoka kifungoni leo, Desemba 27, akionesha nakala la gazeti hilo, alivyokutwa na mpiga picha wetu.
Limerudi tena!!!!
Mwani Nyangassa na Esther Bhoke akiwa wamepozi katika picha, baada ya uchovu wa mizunguko ya leo, makamanda hao wako katika harakati ya kuliuza gazeti hilo ambalo limefunguliwa leo kutoka kifungoni.
Poz kwa Poz, Wafanyakazi wa Newhabari (2006) Ltd, "#TEAM Mauzo"wakiwa wamepozi katika picha ya pamoaja baada ya kuzunguka jiji la Dar es salaam kufanay mauzo ya copy ya gazeti la MTANZANIA.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »