Na Masanja Mabula -Pemba .11/11/2013.
Siku
chache baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Azma Stewart John Hall
kufungasha virago kutoka klabu hiyo , Chama cha Soka cha Zanzibar ZFA
kimesema hakina mpango wa kumuita kocha huyo kwa ajili ya kuifundisha
timu ya taifa ya Zanzibar .
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi , katibu Mkuu wa ZFA Kassim Haji amesema kuwa mpango wa
kumrejesha kocha huyo kukionoa kikosi cha Heroes hakupo na badala yake
wataendelea kumwamini Salum Bausi .
Kassim
amezidi kufahamisha kwamba pamoja na ZFA kuwa ndiyo iliyomleta Stowart
kwa mara ya kwanza hapa nchini , lakini fursa ya kuifundisha timu ya
Taifa ya Zanzibar kwa sasa itakuwa ni ndoto .
"Tunaelewa
uwezo wa Stowart , kwani ndiyo sisi tuliomfungulia milango hapa nchini ,
lakini mipango ya kumrejesha kwa sasa haipo kwani tunawapa nafasi
makocha wazawa " alifahamisha Kassim .
Aidha akizungumzia maandalizi ya timu hiyo ambayo inajiandaa na michuano ya Tusker Challenge Cup
, Kassim amesema kuwa yanaendelea vyema na kupongeza uwamuzi wa kocha wa kuwapima afya wachezaji .
Hata
hivyo alikiri kuwa ZFA inakabiliwa na ukata wa fedha wa kuweza
kuindalia michezo ya kimataifa ya kujipima nguvu kabla ya kuelekea Mjini
Nairobu Kenya kushiriki michuano hiyo .
"Kunahitajika
zaidi ya shilingi milioni 15 , kuandaa mechi ya kimataifa , kwani
tunatakiwa kuigharamia timu ili iweze kufika Zanzibar au timu yetu
kuweza kusafiri , lakini tuna mpango wa kucheza mechi za kirafiki na
vilabu vya Tanzania Bara ikiwemo Kilimanjaro Stars " alieleza .
Awali
uteuzi wa timu ya Taifa ya Zanzibar ulipingwa na wajumbe wa kamati
Tendaji wa ZFA Pemba ambayo nayo ilitangaza kikosi cha wachezaji 30
kuunda timu ya kombaini ya Pemba kwa lengo
la kukutana na iliyochaguliwa na Bausi ili kupata kikosi cha Heroes

EmoticonEmoticon