Na Rahimu Kambi, Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amewashangaa majirani zake, nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kwa kufanya vitendo vinavyoashiria ubinafsi na kuitenga nchi ya Tanzania, bila sababu za msingi.
Rais Kikwete aliyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa
akilihutubia Bunge, ikiwa ni miaka kadhaa tangu alipofanya hivyo mwishoni mwa
mwaka 2010 alipozindua Bunge hilo lilipotoka katika Uchaguzi Mkuu.
Akizingumza kwa hisia kali, Kikwete alisema kwamba pamoja na nchi hizo kutaka kuitanga nchi yake, ila Tanzania itaendelea kuipenda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kamwe haitaweza kuondoka, licha ya dalili za ubinafsi wa Kenya, Uganda na Rwanda kuongezeka.
Rais Kikwete alisema kwamba wao kama wakuu wan chi wamekuwa
wakikutana na kubadilisha mawazo ya kuinga jumuiya hiyo, hivyo inashangaza
kuona wapo watu wanaotaka kufanya mambo yanayoshangaza kwa mustakabali wan chi za
Afrika.
"Na kama wenzetu kuna kosa tumelifanya, nadhani njia nzuri ingekuwa kuwa wawazi na sio kufanya mambo ambayo si mazuri kwa mustakabali wan chi zetu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza Tanzania itaendelea kuwa kwenye jumuiya hiyo na kamwe hawatakuwa tayari kutoka.
Pia alizungumzia mchakato wa kuelekea kwenye Katiba Mpya, akisifia taratibu zote zilizotumika hadi kufikia wakati huu ambapo rasimu ya kwanza imepatikana, huku siku chache zijazo wakitarajiwa kupatikana wajumbe wa Bunge la Katiba.

EmoticonEmoticon