Na Masanja Mabula -Pemba .07/11/2013.
Wadau
wa mchezo wa Kareti Wilaya ya Wete , wameweka bayana mbinu na
mikakati ya kuimarisha mchezo huo ili uweze kusaidia kupatiakana kwa
ajira kwa vijana na kupunguza tatizo ka vijana kutegemea ajira kutoka
Serikalini .
Wakizungumza
kwenye kikao cha kujadili mbinu na mikakati ya kuimarisha mchezo huo ,
uliofanyika kwenye ukumbi wa Jamhuri , wamesema kuwa moja ya mikakati
hiyo ni kuweka viwanja sehemu za wazi ili kuwafanya vijana wengi
kujiunga na mchezo huo .
Kikao
hicho ambacho kiliwashirikisha makatibu na wenyeviti wa vikundi vya
kareti Wilaya hiyo , ambao walipitisha azimio la kufanya bonanza la mchezo huo ili
kuitangaza na kuihamasisha jamii kutambua umuhimu wa mchezo huo .
Afisa
Michezo Wilaya hiyo Suleiman Shavuai , akizungumza kwenye kikao hicho
amewataka walimu wa mchezo wa karati Wilayani humo , kutafuta maeneo ya
wazi na kuacha kufanya mazoezi sehemu za msituni jambo ambalo
linawafanya vijan wengi kushindwa kujiunga na mchezo huo .
Amesema
kuwa mchezo wa karati unaweza kuiletea sifa nchi , endapo vijana
watakuwa tayari kujiunga , huku pia alitoa wito kwa wafadhili kujitokeza
kudhamini mchezo huo .
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake katibu wa kikundi cha Scopion karate gruop cha Ole
, ameitaka jamii kuelewa kwamba mchezo huo ni kama ilivyomichezo
mingine , na kuwataka vijana kujiunga kwa wingi kwa ajili ya kujenga
miili pamoja na kujipatia ajira .
EmoticonEmoticon