RC TANGA AKERWA NA UCHAFU KATA YA USAGARA NA MZINGANI.

October 15, 2013
MKUU WA MKOA WA TANGA AKITOA MAELEKEZO KWA VIONGOZI WA KATA YA MZINGANI NA USAGARA BAADA YA KUKERWA KUTOKANA NA UCHAFUA ULIOKITHIRI MAENEO YA KATA HIZO.
Na Oscar Assenga,Tanga.
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Jiji la Tanga Juliana Malange kuwasimamishia mshahara wa mwezi wa kumi maafisa watendaji wa kata Mzingani na Usagara kutokana na maeneo yao kukutwa yakiwa machafu.

Amesema wasimamishiwe mishahara hiyo mpaka hapo mkurugenzi atakapokwenda kuyakagua maeneo hayo na kuyakuta kwenye hali ya usafi na baadae ampelekee taarifa mkuu huyo wa mkoa ili aruhusu wapewe mishahara.

Gallawa ametoa agizo hilo wakati alipotembelea maeneo hayo kuangalia hali ya usafi ambapo alibaini baadhi ya maeneo kuwa na uchafu uliokithiri na ndipo alipotoa kauli hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kila mara anapopita katika maeneo hayo huyakuta machafu kila siku kitendo ambacho kinalifanya eneo hilo kutokuwa katika mandhara nzuri.

Maafisa watendaji hao ni Said Bendera ambaye ni mtendaji wa kata ya Mzingani na Senyenge Mbaruku wa kata ya Usagara.

Mkuu huyo wa mkoa wa Tanga asema wakati wa ziara yake ya kuzunguka maeneo mbalimbali jijini Tanga mtaa utakaokutwa na uchafu atawajibika Afisa Mtendaji.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwataka maafisa watendaji kuhakikisha wanasimamia kikamilifu suala la usafi katika maeneo yao ili kuyaweka mazingira yao katika hali ya nzuri.

Hata hivyo watendaji hao walimuhaidi mkuu wa mkoa huyo kuwa watahakikisha ndani ya wiki moja maeneo yao yatakuwa katika halai nzuri ya usafi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »