Na Oscar Assenga,Tanga.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu
mkoa wa Tanga (TRBA),Hamisi Jaffary amefanikiwa kutetea kiti chake katika
uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika jana,katika ukumbi wa Bandari mkoani
hapa.
Uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Afisa Utamaduni wa
Jiji la Tanga Peter Semfuko ulikuwa na upinzani mkubwa kwa baadhi ya nafasi
ambazo zilikuwa zikigombewa na wagombea zaidi ya wawili.
Akitangaza matokeo hayo,Semfuko alimtangaza Jaffary
kushika nafasi hiyo baada ya kupata kura 23 za ndio kati ya 24 ambazo zilipigwa
na wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi kwenye wadhifa ambao alikuwa akigombea
peke yake.
Katika uchaguzi huo nafasi ya Makamu Mwenyekiti
ilichukuliwa na Rajab Ahmed “Babla”kwa kupata kura 23 huku kura I ikisema
hapana ambapo pia hakuwa na mpinzani.
Nafasi ya Katibu Mkuu ilichukuliwa na Calistus
Zakaria kwa kumbwaga mpinzani wake Patric Semindu kwa kupata kura 15 kati 6
alizipata mgombea mwenzake.
Kwenye uchaguzi huo nafasi ya Katibu Msaidizi
ilichukuliwa na Gilo Mwanakatwe aliyepata kura 19 kati 2 alizopata mpinzani
wake Said Ramadhani huku nafasi ya mweka hazina ikichukuliwa na Twahiru Mdimu
aliyepata kura 19.
Nafasi nyengine ni wajumbe wa kamati ya utendaji
waliochaguliwa ni Ally Senkole,Hassani Sakala,Omari Kupe na Frank Masumba.
Katika nafasi ya mwakilishi wa wachezaji mkutano
mkuu Taifa kwa mkoa wa Tanga ilichukuliwa na Saa Mumy Mohamed aliyepata kura 14
kati ya 6 alizopat mpinzani wake Adam Issa Semkonde.
EmoticonEmoticon