MWENYEKITI WA JUMUIYA WA WAZAZI CCM MKOA WA TANGA,DR.EDMUND MNDOLWA AKISISITIZA JAMBO WAKATI AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA JUMUIYA WA WAZAZI LUSHOTO. |
KATIBU WA WAZAZI MKOA WA TANGA. |
MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA LUSHOTO,LOTTI AKIZUNGUMZA KWENYE KIKAO HICHO. |
MJUMBE WA HALMASHAURI WA KAMATI YA UTEKELEZAJI WAZAZI MKOA NA MWENYEKITI YA HALMSHAURI YA KOROGWE VIJIJINI,SADICK KALLAGE NAYE AKIZUNGUMZA JAMBO KWENYE MKUTANO HUO |
MWENYEKITI wa Jumiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga,Dr.Edmund Mndolwa amewataka makatibu wa Jumuiya hiyo ngazi ya kata kuvunja makundi na kutokukubali kugawanywa kwa sababu hali hiyo itapeleka mpasuko ndani yao badala yake wawe mstari wa mbele kukilinda chama hicho.
Mndolwa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na makatibu wa wazazi wilaya ya Lushoto ambapo madhumuni makubwa ilikuwa ni kutoa shukrani kwao kwa kumchagua ikiwemo kuzungumzia ujio wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho,Abdallah Bulembo ambaye atafanya ziara yake mkoani Tanga kutembelea shughuli mbalimbali za jumuiya hiyo.
Aidha aliwataka makatibu hao kutokukubali kugawanywa na viongozi wasioitakia mema jumuiya kwani kufanya hivyo kutapeleka wao kushindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa pamoja na kuchangia kuzoofisha maendeleo yao ya kiutendaji kila siku.
"Tusikubali kugawanywa gawanywa kama mahindi au bidhaa sokoni wadhulumu wenu wataadhibiwa wakati wa uchaguzi "Alisema Mndolwa.
Aidha aliwataka kuitunza elimu ikiwemo kuipa kipaumbele na wakubali kuwa elimu ni kitu cha muhimu sana na kuelezea katika shule za wazazi zinahitaji mafanikio makubwa ili ziweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.
Mwenyekiti huyo alisema kwenye shule zao wanahitaji ufanisi mkubwa sana hivyo alimuagiza katibu wake na atailalalisha kwenye kamati ya utekelezaji inayokuja na watatangaza kuwa na sanduku la maoni ambalo litakuwa kwa ajili ya kuwekwa maoni kuhusu ufanisi wa shule za wazazi mkoani hapa.
Alisema aliamua kuweka hivyo kutokana na kuwa wakati mwengine walimu wanaofundisha shule hizo hushindwa kufundisha vema pindi waingiapo darasani na kutomaliza silabasi hali ambayo huchangia kurudisha nyuma maendeleo yao pamoja na wanafunzi wanaofundisha.
EmoticonEmoticon