HAPA AKISALIMIANA NA WAAMUZI ANAYEFUATIA MWENYE TISHETI YA MISTARI NI MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION YA TANGA,HEMED AURORA. |
HAPA MBUNGE WA JIMBO LA TANGA,OMARI NUNDU AKISALIMIA NA WACHEZAJI WA TIMU YA RHINO RANGERS YA TABORA KALBA YA KUANZA MECHI HIYO. |
KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOCHEZA LEO. |
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga leo imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Rhino Rangers ya Tabora ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Ligi kuu Tanzani bara mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Mchezo huo ulikuwa mkali na wenye upinzani wa hali ya juu kutokana na timu zote kushambuliana kwa zamu na kuonyesha kandanda nzuri na la kuvutia ambapo mpaka timu hiyo zikienda mapumziko,Rhino Rangers ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 bao lililofungwa na Salim Majid dakika 26.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Coastal Union union waliwatoa Suleiman Kassim Selembe,Yayo Lutimba,Keneth Masumbuko na kuwaingiza Razack Khalfani,Pius Kisambale na Danny Lyanga ambao waliweza kuubadilisha mchezo huo.
Baada ya kuingia wachezaji hao Coastal Union waliweza kucharuka kwa kucheza pasi fupi fupi na ndefu kitendo ambacho kilipeleka kuweza kufanya mashambulzi mfululizo langoni mwa Rhino Rangers ya Tabora bila mafanikio.
Kwa upande wao Rhino Rangers walionekana kuukamia mchezo huo kwa kucheza kwa umakini mkubwa na ucheza pasi ndefu hali ambayo iliwapeleka kupata nafasi nyingi za wazi na kushindwa kuzifanyia kazi ipasavyo.
Wakionekana kucharuka na kujipanga Coastal Union waliweza kucheza vema katika kipindi pili na kutua baada ya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao na kufanikiwa kuandika bao lao la kusawadhisha dakika ya 81 kupitia Jerry Santo kwa njia ya penati iliyotokana na mchezaji wa Rhino Rangers,Saad Kipanga kuunawa mpira eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo,Jacob Zakaria kuamuru ipigwe penati iliyopigwa kiufundi na Santo na kutinga wavuni.
Katika mchezo wa leo Coastal Union iliwakilishwa na Shaban Kado,Hamad Hamis,Abdi banda,Juma Nyoso,Marcus Ndeheli,Jerry Santo,Suleiman Kassim Selembe,Haruna Moshi Boban,Yayo Lutimba,Keneth Masumbuko na Uhuru Suleiman Mwambugu.
Huku Rhino Rangers ikiwachezesha Abdulkarim Mtumwa,Ally Mwanyiro,Hussein Abdallah,Laban Kambole,Ladslausi Mbogo, Hamisi Msafiri,Nurdin Bakari,Salum Majid,Gidion Brown,Saad Kipanga na Kamana Salum.
EmoticonEmoticon