Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia ambae pia ni Mbunge wa Bumbuli January
Makamba amekata kupokea mradi wa maji wa zaidi ya Sh Mil 400 ambao
ungehudumia vijiji vinne vilivyoko kwenye Jimbo la Bumbuli kutoka na
kujengwa chini ya kiwango.
Hayo
aliyasema wakati akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye kiwanja cha stendi jimboni humo,alisema licha ya
mradi huo kutengewa fedha nyingi na wahisani lakini haukutekeleza vile
ulivyotakiwa.
Alisema
mradi huo ulikuwa uanze kutoa huduma zake kuanzi kijiji cha Kwamanolo
ambao ulikuwa ujenzi unaanzia pamoja na kujenga tanki lenye uwezo wa
kuchukuwa lita lakimoja na thelathini na tano lakini tanki lilijengwa
linachukuwa lita 90 tu
“Nimekata
kuupokea mradi wa maji katika Jimbo langu kutoka na kutoridhishwa na
ujenzi wake lakini pia nimemuomba waziri wa Maji Jumanne Maghembe
atusaidi kuingiza kijiji kimoja katika mradi wa maji uofadhiliwa na
Benki ya dunia wa kuhudumia vijiji kumi ili kupunguza shida ya maji
Bumbuli”alisema Makamba.
Nae
Diwani wa kata ya Bumbuli Tulo Guga alisema kuwa mradi huo ulikuwa
unufaishe vijiji vya Bumbuli Mission,Bumbuli Kaya,Mboki na Kwamanolo
lakini makubaliano ilikuwa kule eneo mradi unapoanzia nilazima maji
yaanze kupatika na pamoja na ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji.
Aliongeza
kuwa yote hayo mkandarasi hakuyatekeleza licha ya kazi ya ujenzi
kukamilika kwa wakati ,lakini kikubwa zaidi ni kujenga tanki ndogo la
kuhifadhia maji ambalo halitaweza kuhudumia wananchi wengi kwa wakati
mmoja.
Hivyo
aliiomba Halimashauri ya Wilaya ya Lushoto kuupokea mradi huo na
kujaribu kurekebisha mapungufu kabla ya kuukabidhi tena kwenye
Hlamshauri ya Bumbuli ili wananchi waweze kunufaika na mradi huo na
kuondokana na kero ya maji .

EmoticonEmoticon