Viongozi wa Dini waaswa

July 19, 2013

Na Mwandishi Wetu,Tanga
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya  dini wametakiwa kuhamasisha mafunzo ya  kuzingatia maadili na matendo mema kwa umini wao kama ambavyo vitabu vya dini hizo  yalivyoamrishwa  ili kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya UKIMWI kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Rai imetolewa na Naibu Meya wa Jiji la Tanga Muzamin Shemdeo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu UKIMWI na Jinsia kwa makundi ya mbalimbali ya kijamii yaliyoratibiwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga kupitia programu ya UKIMWI iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa mipango miji jiji hapa.

Alisema viongozi hao wanajukumu la kuhaisaidia jamii iepukane na ngono zembe kwa kutoa mafunzo yanayohusia na matendo mema ili kuisaidia jamii isiendelee kuangamika katika gonjwa hilo ambalo kwa sasa idadiya maambukizi   inazidi kukua kwa kasi.

“Tunatambua kuna jamii  inayoamini mafundisho ya dini na wengine hata uwaeleze vipi hawana imani hivyo ni vema viongozi wa dini tukashirikiana  katika kuelimishana,na nyie wanahabari tumieni taaluma yenu katika kutoa habari sahihi za ugonjwa huu ili jamii ielimike”alisema Shemdoe.

Nae Mkufunzi wa mafunzo hayo Desideri Joseph alisema mabadiliko ya kijamii yanayotokea ulimwenguni pamoja na nguvu za kiuchumi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuathiri maadili  na tamaduni zetu  kama watanzania .

Alisema stadi za maisha zimekosekana pamoja na hali ya uchumi kuwa duni katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla imekuwa ni kikwazo kikubwa cha udhalilishaji wa kijinsi hali inayopelekea kuchangia maambukizi ya UKIMWI katika jamii nchini.

Hata hivyo Shekhe Shariff Mohamed Yahya alisema uhamasishaji kutumia  wa kondom ilikujilinda  licha ya dini kupinga ndio umekuwa kuhamasisha ngono na kuchangia kasi ya maambukizi mapya kila siku hivyo ni vema jamii ikamrudia mungu ili kupata salama katika gonjwa hilo.

Vilevile Mratibu wa UKIMWI Jiji la Tanga Moses Kisibo alisema kwa sasa kiwango cha maambukizi ni 7.8% huku waathirika wengi wakiwa ni wanandoa na vijana walio katika umri kuolewa ndio kundi linalofuata.

Mafunzo hayo ya siku moja yalihusisha makundi mbalimbali ya watu wakiwemo Viongozi wa dini kutoka taasisi mbalimbali,nakundi ya vijana,wazee,wanasiasa pamoja na waandishi wa habari kwalengo la kuihamasisha jamii juu ya kutambua wajibu wao katika mapambano ya ugonjwa huo.
MWISHO

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »