Ushindi tulioupata Arusha ni ishara ya Kukubalika.

July 17, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Tanga kimesema ushindi walioupata kwenye kata nne za Mkoa wa Arusha katika uchaguzi mdogo wa udiwani mkoani Arusha uliofanyika hivi karibuni ni ishara tosha kuwa chama hicho kinakubalika na wananchi wa mkoa huo.
 
Uchaguzi huo ulifanyika hivi karibuni kwenye kata za Kaloleni,Themi,Kimandulu na Elirahi ambapo chama hicho kiliweza kuchukua nafasi hizo kwa ushindi wa kushindo na kuwabwaga wapinzani wao.
 
Akizungumza na Blog hii, Katibu wa Chama hicho wilaya ya Tanga,Khalid Rashid amesema kuwa licha ya chama hicho kukubalika mkoani humo lakini pia ni ishara tosha kuwa katika ujazo mkuu ujao wa mwaka 2015 vyama vyengine visahau kuchukua nafasi kwenye ukanda wa kaskazini ambapo ndio ngome ya chama hicho.
 
Rashid amewapongeza wananchi wa Arusha  kwa kazi kubwa ya kukiamini chama hicho pamoja na kukupa ridhaa ya kuwaongoza kwani nafasi hiyo inaonyesha ushirikiano ma umoja baina ya viongozi wa kanda na Taifa ilivyoweza kutengeneza mazingira mazuri kuhakikisha wanapata ushindi kwenye uchaguzi huo.
 
Ameongeza kuwa wanaimani kuwa kwa siku zijazo Meya wa Jiji la Arusha atapatikana kupitia chama hicho kutokana na wingi wa idadi ya madiwani waliopo kwenye baraza la madiwani ambapo alisisitiza mshikamano wao ndio ulioleta matokeo mazuri kwa chama hicho.
 
Aidha amesema katika wilaya ya Tanga chama hicho walifanya mikutano sana ya kuhamasisha wananchi kujiunga na chama hicho lengo lilikuwa ni kutengeneza chadema msingi kwa kila mtaa,vijiji na vitongoji ambapo mikutano hiyo waliifanya kwenye kata 7 ambazo ni Mabawa,Msambweni,Duga, Makorora, Central, Chumbageni na Nguvumali lengo likiwa ni kutembelea kata zote 24 za halmashauri ya Jiji la Tanga.
 
Amesema mikutano hiyo ilikuwa na malengo matatu ya kuzungumzia suala la chadema ni msingi na kuzungumzia kuhusu bajeti ya halmashauri ya Jiji la Tanga ikiwemo kupinga kauli ya waziri mkuu ambayo aliitoa bungeni ya sasa hivi watu watakaoleta vurugu wapigwe tu ambapo chama hicho kinaona kitendo hicho serikali haikutenda haki kwa wananchi.
 
Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »