Mfumuko wa bei za Bidhaa masoko mbalimbali jijini Tanga wapanda

July 17, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.

MFUMKO wa bei ya kiungo (Nazi) na vyakula kama Ndizi ya mkono wa Tembo jijini Tanga, umepanda maradufu katika masoko mbalimbali hususani katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Uchunguzi uliofanywa na Blog hii katika baadhi ya masoko ya Ngamiani, Mgandini na soko la Makorora  unaonyesha kwamba wafanyabiashara wengi wamepandisha bei za nafaka hususan nazi na ndizi ya mkono wa Tembo.
Bei hizo zimeonekana kupanda haraka kwa kipindi cha mwezi huu mtukufu wa ramadhani ambapo awali bei ya ndizi ya mkono wa Tembo kikonyo kimoja kilikuwa Sh300 hadi 400, lakini sasa imefika sh800 kwa kila kikonyo kimoja, nazi ilikuwa kati ya Sh300 hadi Sh400 na sasa imepanda na kufikia Sh700 hadi Sh1000 kwa kila moja.
Wakizungumza suala la kupanda kwa bei ya Nazi na ndizi ya mkono wa Tembo baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema licha ya kuwa huu ni mwezi mtukufu wa ramadhani, lakini kinachochangia pia ni kutokana na halisi ya usafiri na miundombinu ya barabara ambako bidhaa hizo zinakotoka.
“Nikweli kuwa kipindi hiki cha mwezi huu mtukufu wa ramadhani watu wengi wa dhehebu la dini ya kiislamu wanashirki kufunga na hata wengine pesa wanazonunulia futari zinawashinda kutokana na kipato wanachopata hakitoshelezi lakini siyo sisi wafanyabiashara ndiyo tunajipandishia bei hapana bali hata huko tunakokwenda kununua wakulima nao wametupandishia bei,” amesema mfanyabiashara wa Nazi na Ndizi ya mkono wa Tembo aliyejitambulisha kwa jina la Josephat.
Aidha wamesema kuwa bei hiyo ya Ndizi ya mkono wa Tembo na kiungo hicho (Nazi) inaweza kupanda maradufu tena kutokana na hali ngumu ya usafirishaji kutokana na kutopatikana kutoka kwa wakulima mashambani.
                                              (Mwisho).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »