KLABU ZA ENGLAND ZIARANI ASIA

May 28, 2013

MAN UNITED, CHELSEA, ARSENAL, CITY, SPURS, LIVERPOOL, SUNDERLAND NDANI YA NYUMBA!!

FERGIE_APOKEWA_CHINAKABLA MSIMU MPYA wa 2013/14 kuanza Klabu kubwa za England zitatirirka Barani Asia kwa Ziara zao za matayarisho lakini pia lengo ni kuteka Soko kubwa huko kwa Klabu zao kwa kujitangaza kwa kishindo.
Arsenal wataanza Ziara yao huko Asia kwa kucheza Jakarta Indonesia Julai 14 na Siku 3 baadae wataenda Vietnam na kumalizia Ziara huko Japan, hii ikiwa Ziara yao ya kwanza Nchini Japan tangu Mwaka 1968.
Huko Japan, Arsenal watacheza na Nagoya Grampus 8, ambayo ni Klabu iliyofundishwa na Meneja wao Arsene Wenger kabla hajatua Arsenal Mwaka 1997, na Mechi hiyo itakuwa Julai 22.
Kisha Arsenal watacheza na Urawa Reds kugombania Saitama City Cup hapo Julai 26 na baada ya hapo kurudi London.
Nao Chelsea, hapo Julai 17 watakuwa huko Bangkok, Thailand kucheza na Kombaini ya Thailand na Tarehe 21 Julai watacheza huko Kuala Lumpur, Malaysia na Julai 25 kucheza Jakarta, Indonesia.
Liverpool watakuwa Australia kucheza na Melbourne Victory na baada ya hapo watapitia Bangkok, Thailand kucheza Mechi moja hapo Julai 28.
Hong Kong itashuhudia Mashindano ya Klabu za Ligi Kuu England kugombea Asia Cup na safari hii washiriki ni Manchester City, Tottenham Hotspur na Sunderland ambao watacheza Mechi zao za Kombe hilo Julai 24 na 27.
Mabingwa wa England, Manchester United, wao watakuwa na Ziara ya Wiki mbili itakayoanza Julai 13 huko Bangkok, Thailand na kisha kuruka kwenda Sydney, Australia na Japan, kucheza na Yokohama F. Marinos na Cerezo Osaka, Timu aliyotoka Shinji Kagawa, na kumalizia Ziara yao huko Hong Kong kucheza na Klabu ya hapo Julai 29.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »