Na
Oscar Assenga, Tanga.
IDARA
ya Uhamiaji Mkoa wa Tanga imeanza kuwaandikisha walowezi wa Malawi na Msumbiji waliokuja
mkoani hapa katika kipindi cha miaka ya nyuma ambao walikuwa wakifanya kazi
kwenye mashamba ya mkonge na kazi za majumbani.
Akizungumza
na blog hii, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Sixtus Nyaki alisema uandikishwaji
watu hao unafanyika baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kuwaelimisha kwa
kushirikiana na wenyeviti wa mitaa, vitongoji na maafisa watendaji wa kata na vijiji.
Nyaki
alisema wakati wakiwa wanaendesha zoezi hilo wanakumbana na changamoto
mbalimbali ikiwemo baada yao kutokukubali kuandikishwa kwa kuona kama
wanafukuzwa hapa nchini hali ambayo inapelekea kuwa na ugumu kiasi.
Alisema
katika kupambana na wimbi la uhamiaji haramu mkoani hapa idara hiyo imefungua
ofisi ya uhamiaji wilayani Korogwe lengo likiwa ni kuzibiti ongezeko la
wahamiaji wanaoingia mkoani hapa kutoka nchi mbalimbali duniani.
Ofisa
huyo alisema ofisi hiyo itakuwa na kazi ya kuwahudumia wilaya ya Korogwe na
wilaya ya Lushoto wakati idara hiyo ikiendelea kujipanga kwa ajili ya kufungua
ofisi nyengine wilayani humo ikiwa ni mkakati wa kupambana na wahamiaji haramu.
Aidha
alisema tayari wameshapata ofisi hiyo na ukarabati wake unaendelea ambapo
unatarajiwa kukamilika muda sio mrefu ili iweza kufanya kazi zake ambapo
aliongeza kuwa idara hiyo pia imeweka vizuizi katika barabara za
Tanga-Horohoro, Tanga-Arusha na Tanga-Dar.
Hata
hivyo aliogeza kuwa wataendelea kutoa elimu ya uhamiaji shirikishi kwa wananchi
katika maeneo mbalimbali lengo likiwa ni kupunguza wimbi la wahamiaji haramu
mkoani hapa pamoja na kuweza mikakati ya kupunguza uwepo wapo.
Mwisho.
EmoticonEmoticon