HALL: Aipigia saluti Coastal Union.

April 28, 2013
Oscar Assenga, Tanga.

KOCHA Mkuu wa Azam Fc,Stewart Hall amesifu kiwango cha timu ya Coastal Union ya Tanga kwa kueleza wachezaji wake wana uwezo mkubwa wa kuipa mafanikio timu hiyo siku zijazo.
Akizungumza na Blogi hii mara baada ya kumalizika mechi kati yao na Coastal Union ambapo timu zote zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 ,Hall alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu na yenye ushindi kutokana na kila timu kuonekana kujipanga vema hasa katika mzunguko huo wa lala salama.
Hall alisema licha ya wao kujipanga vilivyo kuweza kuibuka na ushindi lakini hali haikuwa kama walivyotegemea kutokana na timu waliokuwa wakicheza nayo kuonekana kujipanga zaidi.
“Matarajio yetu ilikuwa tushinde ili kuweza kuongeza nafasi yetu ya kupata ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara na sio vyenginevyo “Alisema Hall.
Kwa upande wake,Kocha Mkuu wa Costal Union,Hemed Morroco alisema wanamshukuru mungu kwa kupata pointi moja muhimu na kueleza hivi sasa nguvu zao watazielekeza kwenye mechi yao na Yanga.
Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »