Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
amesema licha ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi licha ya kuleta maendeleo kwa
wananchi ikiwemoujenzi wa barabara bora ambazo wanazitumia lakini bado
wanaibeze serikali iliyoko madarakani.
Hayo aliyeasema wakati akizindua mradi wa barabara ya
lami ya Tanga Horohoro yenye urefu wa Km 65 katika eneo la Kasera kwenye
wilayani Mkinga Mkoani Tanga, alisema wapinzani kazi yao ni kubeza maendeleo
yanayofanywa katika nchi .
Alisema mwaka 2010 alipokuaja mkoani hapa kuomba kura
aliwahakikishia wanachi kuwa mradi huo barabara utakamilika kabla ya kuondoka
madarakani ambapo kwa wapinnzani ilikuwa ni vijembe kwenye majukwaa ya kisiasa
kuwa ni ndoto ujenzi huo kukamilika.
“Leo nazindua ujenzi wa barabara ambao umeshirikisha
serikali ya Tanzania na na Marekani kupitia mfuko wake wa Changamoto za Milenia
MCC,lakini yote haya wapinzani hawataona kuwa ni maendeleo bali mwenye nyoyo za
korosho hawewezi kutusifia na kutupongeza”alisema Kikwete.
Hata hivyo alisema ujenzi huo uligharimu kiasi cha
dola Bil 75.75 hadi kukamilika kwake kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa
madaraja 11 na alama za barabara ikiwemo kingo na maenero ya waendakwa miguu .
Rais Kikwete alisema lengo la serikali ni kuunganisha
mtandao wa barabara kuu nchi nzima kuwa za kiwango cha lami na zinazopitika
katika maira yote ya mwaka ili kurahisisha usafirishaji pamoja na kuchangia
kasi ya maendeleo katika nchi.
Nae Balozi wa Marekani Nchini Alfonso Lenhardts
alisema kukamilika na kuzinduliwa kwa barabara hiyo kutasaidia fursa za
biashara kati ya Tanzania na nchi za Kenya ,Msumbiji na Nchia ya Malawi na
kuleta maendeleo kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara hizo na taifa kwa
ujumla.
Alisema serikali ya Marekani imetenga kiasi cha Dol
Mil 698 kwa ajili ya kusaidia miradi ya barabara,nishati na mifumo ya maji
ikiwemo kukarabati Km 435 za barabara nchi ili kuweza kuwa na mtandao wa
barabara za lami.
“Watu wa Marekani kupitia Rais Barack Obama
tunaifuvunia ufadhili huu kwqa ushirikiano na serikali ya Tanzania Kuchangia
kuboresha mtandao wa barabara nchini Tanzania utakaovutua wawekezaji na
kuchangia pato la taifa la nchi hii”alisema Balozi wa Marekani.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa alisema
wananchi wa Tanga wataitunza barabara hiyo kwa kuhakikisha wanazingatia
matumizi sahihi ya barabara ikiwemo kutoruhusu magari yenye uzito mkubwa pamoja
kuchoma moto kando ya barabara.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Patrick Mfugale
alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua milango ya biashara katika nchi
za Afrika ya Mashariki na kutawezesha wafanyabiashara kutumia bandari ya Tanga
kwa ukamilifu.
Mwisho.
EmoticonEmoticon