WAGANGA WAFAWIDHI WATAKIWA KUTENGA BAJETI KUNUNUA MAFUTA YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI.

February 13, 2024

 Na Janeth Raphael - MichuziTv DODOMA.


Waganga Wafawidhi wa vituo vya huduma za Afya msingi Nchini wametakiwa kutenga Bajeti ya ya fedha,katika kila mwaka wa fedha kwaajili ya kununua mafuta ya kuwasaidia watu wenye Ulemavu wa ngozi(Albino)

Maagizo hayo yametolewa Jijini Dodoma na Naibu waziri TAMISEMI anayeshughulikia mambo ya afya DKt Festo Ndugange katika Mkutano wa mwaka wa Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutokea huduma za Afya ngazi ya msingi uliofanyika Jijini hapa.

Na kuongeza katika miaka mitatu ni Halmashauri 47 tu zilizotenga Bajeti hiyo kwa huduma ya mafuta kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.

"Ndugu zangu Waganga Wafawidhi utengaji wa Fedha ya mafuta kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi ni maelekezo ya Serikali na ni muhimu Sana, katika kipindi cha miaka mitatu ni Halmashauri 47 tu zilitenga fedha za mafuta kwa ajili ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (ualbino),kwahiyo niwaombe tuhakikishe kwenye vituo vyetu tunawatambua watu wenye Ulemavu wa ngozi".

" Ndugu Waganga Wafawidhi tengeni Bajeti kwaajili ya vifaa saidizi kwa watu wenye mahitaji maalum na mafuta kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi,pia kutoa mafunzo kwa watoa huduma wa Afya jinsi ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum".

Aidha Naibu Waziri amewataka Waganga Wafawidhi hao kujitathmini na kujiuliza maswali kama wanatatua changamoto zinazowakabili wanachi ipasavyo,kwa weledi na kwa wakati.

"Kuna Malalamiko ya wananchi wanakuja kulalamika kuwa kuna Watumishi wanatoa lugha ambazo sio mzuri ,au kasema hakuna dawa na dawa zinapatikana au alitakiwa kuwa kazini na hayupo hivyo Maswali ambayo tunapaswa kujiuliza ni Je tunatatua changamoto za wananchi ipasavyo,kwa weledi na kwa wakati. Hapa tupate majawabu na kuondoka na maazimio ya kwenda kuboresha mapungufu na Malalamiko yaliyopo".

Sambamba na hayo yote pia hakuacha kuwa kumbusha Waganga Wafawidhi katika suala la utunzaji wa vifaa Tiba ambavyo Serikali inanunua na kupeleka katika vituo vya Afya kwani Serikali inatumia mabilioni ya fedha.

"Wakati mwingine unakuta vifaa Tiba vimewekwa katika sehemu isiyo salama na yenye vumbi wakati vifaa hivyo ni vya mabilioni, na sisi Waganga Wafawidhi tumepewa dhamana hiyo ya kutunza vifaa hivyo kila Mmoja akasimamie suala la utunzaji wa vifaa".

Naibu Waziri amesisitiza pia kuwa Serikali haita sita kumchukulia hatua Kali au hata kumfutia leseni ya Kazi yeyote atakaye kiuka Maadili ya Kazi yake.

Akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Waganga Wafawidhi, Dkt Florence Hilari Mwenyekiti wa Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya msingi Tanzania Bara ameahidi kuyatekeleza maagizo yote ikiwemo kutenga Bajeti kwaajili ya wenye mahitaji maalum, yaliyotolewa na Serikali kupitia Naibu Waziri.

"Kwa niaba ya Waganga Wafawidhi wenzangu tunakushuruku na tunakuahidi kuyatekeleza haya na kuyasimamia kwa weledi mkubwa kama ilivyo kauli mbiu yetu".

Hii ni moja Kati ya mikutano ya Waganga Wafawidhi ambayo hufanyika kwaajili ya kukumbushana na kujengeana uwezo ili kuleta ufanisi na tija katika Kazi.
 

Naibu Waziri TAMISEMI anayeshughulikia mambo ya Afya Dkt. Festo Dugange akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi uliofanyika Leo Februari 13, 2024 Jijini Dodoma.
 

Dkt. Florence Hilari Mwenyekiti wa Waganga wafawidhi wa vituo vya huduma za afya Msingi Tanzania bara akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi uliofanyika Leo Februari 13, 2024 Jijini Dodoma.
 

NAIBU Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Dkt.Wilson Mahera, akizungumza na Waganga Wafawidhi wakati  akifungua  Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe,akizungumza wakati  wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
 

MGANGA Mkuu (RMO) wa Mkoa wa Dodoma Dk. Best Magoma,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.


 

SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange (hayupo pichani), akizungumza wakati  akifungua  Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »