NAIBU WAZIRI MWINJUMA ATOA MAAGIZO TAMRISO

December 20, 2023

NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' ametoa maagizo matatu kwa Kampuni ya kukusanya na kugawa mirabaha (Tamriso).

Maagizo hayo ni kutoa elimu kwa wasanii wa muziki, wakusanyaji na wanaokusanyiwa mirabaha kabla ya kuanza zoezi la ukusanyaji mirabaha January 14 mwakani.

Akizungumza Leo Disemba 19,2023 alipofanya ziara katika ofisi ya Tamriso Mikocheni Jijini Dar es Salaam,amesema kabla ya ugawaji wa mirabaha elimu inatakiwa kutolewa kwa watu hao wawili, waweze kufahamu na kuepuka malalamiko.

Ameeleza kuwa Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali ambazo wameziwasilisha kwake na ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mara kwa mara.

"Ziara yangu katika ofisi ya Tamriso kwa lengo kujadiliana namna kazi ya kusanyaji wa mirabaha."

Amefafanua kuwa muda si mrefu wasanii wataenda kunufaika kutokana na kazi zao.

Mwenyekiti wa Tamriso, Jane Gonsalves amesema watahakikisha wanazingatia maagizo waliyopewa na Naibu Waziri kwa lengo kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mirabaha.

"Utoaji wa elimu kwa wasanii, wakusanyaji wa mirabaha na wanaokusanyiwa utafanyika na utakuwa utakuwa endelevu kufanyika.''

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »